[ad_1]
Watoto wa MUNGU jambo lingine ambalo nitakuja kuongea katika kitu kinachoitwa Christmas tree ni nini na asili yake ni nini. Napenda kukuuliza kwanza ndugu msikilizaji, Biblia imeandika Christmas tree? Christmas ni nini? Christmas ni birthday ya BWANA YESU wa Nazareti peke yake. Sasa inapokuwa imewekwa Christmas tree, ina maana kuwa YESU amenyang’anywa birthday yake. Na zaidi, hakuna mti wa Christmas. Christmas ni birthday ya BWANA YESU peke yake, Mfalme wa wafalme, mwana wa MUNGU ambaye jina lake tunalitukuza tunamwita YESU.
BWANA YESU asifiwe, sasa shetani akaja, akaingilia ili awateke wana wa MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Christmas tree maana yake ni mungu mmea ambaye yuko huko kuzimu ambapo hapo zamani watu wa huko Uingereza, BWANA YESU asifiwe; walikuwa wanaufanya huo mti kama ni MUNGU. Kila wakiona wakila vitu vya kijani walikuwa wanaamini maisha yao yanasonga mbele wanakuwa na uhai. Kwa hiyo wakaona mti wauite mungu unaitwa tammuz. BWANA YESU asifiwe, Haleluya… Sasa tammuz hilihili, ndilo likaingizwa kwenye siku ya birthday ya BWANA YESU wakasema huu mti uitwe Christmas tree ili kuchukua nafasi ya BWANA YESU kama ilivyoibiwa; ikachafuliwa.
BWANA YESU asifiwe. Sasa ile siku ya Christmas watu wanakuwa wameweka ule mti ndani kumbe wanakuwa wamemweka mzimu wa tammuz na nilipokwenda kuzimu mimi tammuz nilimuona. Ni limzimu likubwa lina mandevu, na likubwa kama li-mbuyu, BWANA YESU asifiwe; ili kwamba kuhakikisha kwamba, wana wa MUNGU siku ya Christmas YESU asipite kuzibariki nyumba zao, kutembea na kushiriki nao. Zaidi, unapoweka ule mti, unakuwa umemsujudu mzimu anaitwa tammuz na kule kuzimu pia wanasherehekea pia siku ya Christmas; lakini wanavyosherehekea wao, wanaweka ule mti vile vile ndani ya nyumba, imeitwa Christmas tree. Sasa unavyoweka Christmas tree, na wewe mwanadamu unaunganishwa huko, tayari umeunganishwa na mizimu.
BWANA YESU asifiwe. Ni ajabu sana hata makanisani hiyo miti imejaa, YESU angemtuma nani? Wangemweleza nani? Kwa sababu wamekimbilia pesa, hawataki kumsikiliza BWANA YESU. Mimi nawaeleza ukweli kwa sababu watu wamefanyika kuasi pasipo kupenda, na wengine hawajui; hata mimi nilikuwa najua Christmas tree ni kitu kizuri. Ninakuambia, tupa, kachome. Hakina uhusiano na BWANA YESU. Haleluya… BWANA YESU peke yake ndiye unatakiwa umwamini na usherehekee siku ya Christmas umpambe katika roho yako na moyo wako. Lakini cha ajabu siku hizi miungu ndiyo inayokuwa katika makanisa. Tazama miezi ya 12, tazama watu wameficha na manailoni yametengenezwa na mataifa mbalimbali. Imeweka mzimu unaitwa tammuz huko kuzimu. Madhara yake, unakuwa umemwasi MUNGU, umemwasi BWANA YESU, umemwasi ROHO MTAKATIFU na wote watatu na YESU hayuko kwako. Sasa imefichwa katika ulimwengu wa roho, matokeo yake wewe umemwabudu tammuz mungu mmea pasipo kujua na wengine wanajua. Ni ajabu sana. Tazama kwenye makanisa miezi ya 12 yamejaa kwenye mahoteli sehemu mbalimbali wanasema Christmas tree. Wewe birthday ya YESU haipambwi kwa mti, inapambwa kwa utakatifu na kumshukuru na kumsifu ndani ya moyo wako wewe, sio katika mti. Sasa shetani akaiba uthamani wa Christmas akaweka mti. Aliiba katika mambo mawili ambayo nitakwenda kuelezea. Jambo lingine ni father Christmas, lakini nina-base (ninasisitiza) katika jambo la Christmas tree. Unapokuwa umenunua ule mti tu, ina maana wewe una aina ya mungu anaitwa tammuz; tayari wewe umeshamwasi MUNGU. Lakini hii sio kwamba watumishi wa sasa hivi walipenda; walitekwa na wale watumishi wa zamani ambao waliacha njia ya YESU, wakawaua kina Paulo, BWANA YESU ASIFIWE, na wanafunzi wa YESU; wakaingiza mambo yao na niliwakuta huko kuzimu toka wale watumishi wa enzi ya Ufilipi walioharibu Injili. Wakati huo kuna makanisa machache ambayo yalikuwa yanasema ukweli, sasa hivi yamejaa mengi ambayo ni uwongo. Ni pesa, uwongo na kutafuta pesa za wana wa MUNGU.
BWANA YESU asifiwe, nikuulize mwana wa MUNGU, muulize mchungaji wako ni kwa nini wanaweka huo mti? Hana jibu. Muulize maswali, na kama hajui, basi. Which GOD anamwabudu? Hajui. Kama wewe vile ulivyo unaabudu mungu usiyemjua badala ya kumwabudu MUNGU unayemjua, aliyekuumba, aliyeumba mwezi, nyota na jua pamoja na kila kitu.
BWANA YESU asifiwe. Hii miti haipaswi kushiriki utukufu wa MUNGU au wa YESU, wala kiumbe chochote. Hafananishwi, anaitwa mwana wa pekee. Kama ni mwana wa pekee, leo hii iweje mti uwekwe hapa uchanganywe na mwana wa pekee? Lazima uelewe. BWANA YESU asifiwe. Ni wakati wa kumjua YESU na wakati wa kumjua MUNGU wa kweli, na ni wakati wa kweli tupu mpaka atakapokuja. Unayesikia utapona, unayekaza shingo shauri yako; lakini sitadaiwa damu yako katika mikono yangu, na MUNGU damu yako haitamlilia katika mikono yake. Wakati ni huu sasa kuna wengine hawatendi dhambi lakini hawajui ni mahali gani wameanguka.
BWANA YESU asifiwe. Unapokuwa na Christmas tree, miungu, majini, mapepo yapo nyumbani kwako; iwe umeokoka, haujaokoka ukweli ndio huu. Uamue leo. BWANA YESU asifiwe. Katika kabila ya Uchagga niliyotoka, miti imejaa ya Christmas; yaani tammuz ndio limekamata. Ninawaambia watupe katika jina la YESU. Nimekufundisha, chagua leo unataka miungu au unamtaka BWANA YESU? Na YESU anakukodolea macho yake kutoka mbinguni, anakuona wewe mwanadamu unasikia, na siku yake ile ya Christmas unakwenda kuwapa miungu badala ya yeye. Inatakiwa umrudie yeye mwenyewe; mambo yameharibika watoto wa MUNGU; kanisa limetekwa na shetani limepoteza direction (mwelekeo) halisemi kweli. Mambo ni mengi sana ninayowafundisha, lakini bado sijaanza kufundisha, hii ni mwanzo. BWANA YESU asifiwe, Haleluya,… acheni mambo ya miungu, nimekueleza habari ya Christmas tree, sasa umeelewa.
BWANA YESU asifiwe. Jambo lingine tena naeleza ni kuhusu kitu kinaitwa father Christmas. Kama nilivyokwisha kuwaeleza kwamba Christmas tree ni makosa, na tukisema father Christmas; hivi nikuulize; father Christmas ni nani? YESU au ni mdoli, YESU au ni hiyo sanamu? Wanadamu ni namna gani mmetekwa fahamu badala ya kumtukuza YESU baba yetu tukatengenezewa midoli halafu tukaiita father Christmas. Sasa ninakupa siri kidogo ya asili ya father Christmas. father Christmas ni mzimu wa mtu anaitwa Saint Nicholas. Alikuwa ni mtu maarufu sana zamani katika nchi za Ugiriki na Uturuki, alikufaga. BWANA YESU asifiwe. Baada ya kufa kwa sababu alikuwa na matendo mazuri, BWANA YESU asifiwe. Ndio wakampa jina wamuite father Christmas. Sasa leo hii amekufa, hivyo kila unapokuwa na huyu mdoli unaoitwa father Christmas, unapeleka watoto, hata yule mtu amevaa lile linguo anacheza cheza ajue kama huyo mtu tayari ameshavaliwa na huyo mzimu linaitwa Saint Nicholas. BWANA YESU asifiwe, sasa ni kuelewa kwamba mambo yameharibika. YESU siku yake ya kuzaliwa imechafuliwa, badala ya kutukuzwa yeye amepewa mdoli ambaye anaitwa Nicholas ambaye sasa hivi ni mzimu. Sasa watu wanaacha kumtukuza YESU na kumsherehekea yeye katika roho na kweli. Shetani akatengeneza kitu akasema, ngoja wanadamu nimewashika fahamu zao niwaambie huyo ndio father Christmas. Nikuulize swali, huyo mdoli ndiyo BABA YESU? Jibu siyo. Na nikuulize swali, je inastahili huo mdoli uitwe father Christmas? Tazama ni pepo lina mandevu, lina manywele, hata watoto wakiona wanaanza kucheka na mavidole makubwa kama jini. Ni namna gani Wakristo, ni wakati wa kumrudia MUNGU. Mambo yameharibika, yalianzia ulaya, Injili imebadilika, na makanisa yamepigwa upofu, hayajui ukweli. Kanisani yenyewe kwenda, utakuta ni lipepo limekaa. Hivi mnajua midoli ndio mapepo yanakaa? Na leo ndio anaitwa father Christmas badala ya YESU kurudishiwa utukukufu peke yake na MUNGU kushukuriwa kwa sababu ametuletea YESU. BWANA YESU ASIFIWE. Ninawatangazia katika ulimwengu mzima, hakuna mtu anatakiwa kuitwa father Christmas, hakuna kitu kinatakiwa kuitwa Christmas tree; ni YESU peke yake birthday yake na kutukuzwa MUNGU kwa kazi aliyoifanya kutuletea Mfalame wa wafalme, Bwana wa wafalme. Kupitia jina lake leo sisi sote tumekombelewa na tunaenda mbinguni. Iweje leo shetani anakamata fahamu za wanadamu akachomeka Christmas tree iitwe Christmas, akaleta mdoli uitwe Christmas. Ni sawasawa na hawa amabao wanajiita YESU, ni wakati wa kukataa. Ni sawasawa na hawa ambao wanajiita mungu wa majeshi, ni wakati wa kukataa. BWANA YESU asifiwe. Ninawaambia mambo yameharibika; kama leo hii mtu wanasema wao ni Adam wa pili, kesho kutwa utasikia mtu anasema yeye ni Adam wa kwanza wakati Adam wa pili ni YESU peke yake. Watu wanachukua nafasi za BWANA YESU. Ni wakati wa kusimama imara kama unampenda MUNGU.
BWANA YESU asifiwe. Amenituma habari njema kwa mataifa yote kuwaeleza ukweli, kufungua fahamu zenu na akili zenu kwa sababu kila unapokuwa na yule ndoli, shetani hata siku unakufa anakunyanyulia bango wewe uliabudu sanamu siku ile ukamuita father Christmas. Nikufundishe wewe Mkristo na wewe mpagani; Je YESU ndilo hilo limdoli? Je siku ya kuzaliwa ndio inaitwa mti wa YESU? Hakuna mti wa YESU hapa duniani. BWANA YESU asifiwe. YESU peke yake hafananishwi na chochote ndio anaitwa mwana wa pekee hata miti na viumbe vya MUNGU.
BWANA YESU asifiwe, lakini shetani akaamua kuwateka wanadamu wamkosee MUNGU, hata mti waite ni mungu wao. Lakini uliza, miungu haina kuitu, hata mmea kuupa pumzi, kuinyeshea. Miungu hata mvua haidondoshi. BWANA YESU asifiwe; haijatoa ila ni MUNGU lakini kanisa limeenda kinyume na kupoteza ramani; wamejiita, ni wazinzi, wananyang’anya watu pesa, mali na kudanganya danganya watu kwa injili za upotofu. Ni theolojia gani hizi? Soma katika kitabu cha Biblia takatifu ambayo ndio katiba; hakuna mtu anayeruhusiwa kuwa father Christmas. Mwana wa MUNGU hafananishwi na chochote. Sasa iweje leo mwana wa MUNGU afananishwe na huyo mdoli? Iweje leo mwana wa MUNGU anafananishwa na mti? Siku yake ni siku tofauti. Unapoweka tammuz, unapoweka hilo li father Christmas; linaitwa father Christmas la kuzimu, maana kuzimu na wenyewe wanalo; unapoliweka siku hiyo, YESU ndiyo hahusiki na nyumba yako, wala baraka zake hazishuki kwako. BWANA YESU asifiwe. Zaidi ile mizimu kule kuzimu inachekelea inasema “majinga haya”. Mimi YESU alinipeleka nikaona yote na ninawafundisha, ninawaeleza, anayesikia asikilize. Mimi nina uadui na shetani, na shetani kila siku tunagombana, na tutagombana milele, na ninaendelea kumtandika na uendelee. Najua mpaka sasa wengi mmefunguka na fahamu zenu zinazidi kuelewa. Uelewe macho yako yafunguliwe, na fahamu zako zifunguliwe uwe na akili timamu. Yamkini umesoma, na una digrii (shahada) tatu, nne, lakini kwa nini huelewi father Christmas huyu sio YESU? Hii Christmas tree sio YESU ni dhambi. Haleluya,…
Zaidi karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI, shida yoyote inayojusumbua, matatizo yote, njoo utafunguliwa bure bila hata senti kumi. Amenituma YESU niwaeleze ukweli dunia nzima. Tazama siku ya Christmas miezi ya 12 ni wakati wa kumwasi MUNGU. Kuweka mamidoli haya ni kumwasi, kuweka ma-christma tree ni kumwasi. Yamkini na wewe mwana wa MUNGU hupendi kumwasi MUNGU lakini unafanyishwa kumwasi kwa namna hii. Jichunguze unaye huko ndani ujue umemwasi MUNGU; wewe ni kuyatoa nje, kuyatupa na kuyakataa. Na madukani wafanyabiashara mnapoyauza, mjue. Kama mlikuwa hamuelewi sasa muelewe. Msifanye kazi ya kumuudhi MUNGU mnapoleta hivyo vitu. Mnampenda MUNGU, lakini inapitishwa kwenye mikono yako; mmepigwa upofu. Watu wamepigwa upofu wanaleta vitu vya shetani kwenye mikono yenu. Mnasubiri baraka, huwezi kupata baraka za MUNGU. BWANA YESU asifiwe; Haleluya… Ni wakati wa kufunguka na kujua ukweli. Atukuzwe MUNGU wa Ibrahimu, MUNGU wa Isaka.
Sema BWANA YESU, naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua au kutokujua, ninamkataa shetani na kazi zake zote. YESU unishike, na jina langu liandike, nibadilishe maisha yangu, ROHO wako MTAKATIFU aniongoze nisitekwe na shetani. Unapokuja usiniache, uniongoze mahali ulipo wewe, nikutane na wewe, nisinajisike, nakushukuru. Sitaweka Christmas tree, sitaweka hilo li father Christmas – lipepo katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti. Nakushukuru kwa kuniponya. Tutaonana muda mwingine tena wakati kama huu, MUNGU akubariki. Zaidi karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI, fuatilia masomo katika blog (prophethebron.blogspot.com), utakuta masomo haya zaidi kwa undani na vitabu na DVD. Soma, usikilize. Amani ya MUNGU ikae na wewe. Ubarikiwe. Bye.
NABII HEBRON.
[ad_2]