[ad_1]
Nabii Hebron: BWANA YESU asifiwe, ndugu mtazamaji na mtazamaji na mtoto wa MUNGU na mwanadamu uliyeumbwa na MUNGU, siku ya leo ninayo habari njema ambayo ninakuletea kwa njia ya shuhuda ambayo ni mtoto ambaye aliyekuwa kuzimu na ambaye alikuwa ni namba tatu katika ufalme wa shetani. Namba moja ni joka kuu, namba mbili ni shetani ambaye ni lusifa na namba tatu ni roho mchafu wa kuzimu.
Shetani pia naye katika ufalme wake aliiga kama vile vile mbinguni. Kwa hiyo joka kuu ndiye mungu, shetani ndiye mwana wa pekee na roho mtakatifu ni roho mchafu. BWANA YESU asifiwe.
BWANA YESU asifiwe. Kijana huyu ambaye muda sio mrefu nitawaletea habari zake na tuko naye hapa, nitafanya naye mahojiani ambayo yatakujenga na yatakujenga na yatakusaidia baada ya kutumwa kwangu kuja kuniangusha ikashindikana, na leo hii ni mtoto wa YESU ameokoka, anamtukuza BWANA. BWANA YESU asifiwe. Amen
Max ambaye sasa anaitwa jina Isaya naye ajitambulishe kabla ya mahojiano yetu. Karibu Isaya.
Isaya: Asante, BWANA YESU asifiwe, mimi kwa jina naitwa Max jina langu la kwanza, lakini jina langu la sasa hivi naitwa Isaya. Ni mtoto ambaye Nabii Hebron alikuwa anamuongelea. Anachokisema ni kweli, nilikuea natumika kuzimu ambaye nilisimama kama namba tatu; baada ya joka kuu, lusifa na mimi mwenyewe. Lakini sasa hivi nimeokoka, nampenda YESU na nimeamua kurudi kwa MUNGU.
Nilienda kuzimu nikiwa mtoto mdogo; niliishi maisha ya huko; sikuweza kukaa na kuongea na binadamu lakini MUNGU mwenyewe mipango yake kwa kwa sasa nimetoka huko na ni mtoto wa MUNGU, nampenda YESU.
Nabii Hebron: Karibu sana Isaya, mtoto wa MUNGU.
Isaya: Asante.
Nabii Hebron: Sasa tutafanya mahojiano kidogo, katika yale ambayo nitakuuliza, na mengine utaeleza tu, kwa sababu wewe ulikuwa ni mshiriki mkuu wa lusifa na joka kuu na mficha siri zote za shetani ambazo alizokuwa anazipanga kwa ajili ya ulimwengu huu, na kwa ajili ya watu wote hata wewe ndugu mtazamaji unayeangalia. Lakini leo hii hapa tuko naye ambaye anafichua siri zote ambazo alizokuwa amezipanga, kwa hiyo ni wewe kusikiliza. Nitakuuliza ilikuwaje, ulipelekwaje kuzimu na ulikuwa unafanya kazi gani tutaenda hatua kwa hatua na uliishi miaka mingapi kuzimu.
Isaya: Niliishi miaka kumi na nne (14)
Nabii Hebron: Unakumbuka jinsi ulivyopelekwa?
Isaya: Kwa kweli sikumbuki, ila nilivyopata ufahamu vizuri nikajikuta niko naishi kule.
Nabii Hebron: Na kule kuzimu ulikuwa unafanya kazi gani, au baada ya kufika kule walikupa kazi gani?
Isaya: Kiongozi. Nilikuwa kiongozi wa kusimamia majeshi yote ya majini, mapepo na wachawi na watu wengine ambao wamekwenda kinyume na MUNGU kule kuzimu. Mimi ndio nilikuwa msimamizi wao.
Nabii Hebron: Unaposema usimamizi unakuwa unasimamia ili nini? Au katika kuwapa nguvu au kiongozi wao?
Isaya:Kwa kweli katika vyote:
Nabii Hebron: Katika vyote?
Isaya: Kuwapa nguvu, na kuwasimamia hata katika kazi tukiwa tunaangalia kazi ambayo atatunga baba wa kule kuzimu ambaye ni joka kuu mwenyewe, akishirikiana na lusifa. Amri ikitoka kwa joka kuu inatakiwa ifanyike. Kazi hii inafikishwa kwa lusifa “then” (halafu) inafika kwangu.
Nabii Hebron: Kwa hiyo ikishafika kwako lazima itimie?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Na hakukuwa na mwanadamu yeyote ambaye alikuwa ametekwa na akaweza kupewa nafasi ya cheo kama cha kwako?
Isaya: Hapana.
Nabii Hebron: Na unaweza kunielezea au ndugu watazamaji cheo chako kilikuwaje au ulikuwa nfana una nyota ngapi au una nini?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Karibu, endelea.
Isaya: Cheo change kilikuwa ni kuiteka dunia. Hicho ni cheo change cha kwanza ambacho nilipewa kuteka ulimwengu mzima uingie kuzimu na usiende kwa MUNGU.
Kazi yangu ya pili niliyokuwa nimepewa ni kusimamia majeshi yote ya kuzimu na watu mbalimbali ambao wana vyeo kule kuzimu, na kusimamia wachungaji wote na manabii.
Nabii Hebron: Manabii na wachungaji wa namna gani?
Isaya: Wa kipepo tuseme.
Nabii Hebron: Hao wa kipepo ina maana wako duniani lakini wako kule chini?
Isaya: Ndiyo, ndiyo.
Nabii Hebron: Na walipokuwa ukiwasimamia hapa duniani unawajua?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Unawajua kabisa?
Isaya: Nawajua.
Nabii Hebron: Ni nguvu gani ilikuwa inatenda, na ni namna gani hiyo nguvu inavyokuwa inatenda kazi wapohubiri?
Isaya: Linatumwa pepo moja, linasimama mahali anapokuwa anahubiri, yaani tuseme madhabahuni pale. Lile pepo linakuwa linatoa nguvu ambazo ni nguvu za kipepo. Ndio maana mnaona mtu anapoguswa kichwa anaanguka lakini ukifuatilia katika ulimwengu wa roho anakuwa anapewa pepo na nyota yake pia huchukuliwa.
Nabii Hebron: Na hii habari ya misukule inakuwaje, maana na hiyo uliniambia pia? Kwa habari ya mtumishi anayekfufua misukule na anasema yeye ni mtumishi wa MUNGU na anataja jina la YESU. Hapo inakuwaje?
Isaya: Ile misukule anayokuwa anaifufua haifufuki yenyewe, huwa anaingiza roho ya pepo yoyote inakuwa inakaa ndani ya yule mtu, anavyoitamkia kitu lile pepo linaamka.
Nabii Hebron: Linatii?
Isaya: Ndiyo
Nabii Hebron: Halafu huku duniani watu wanaona ni mtu amefufuka?
Isaya: Wanaona ni mtu kafufuka
Nabii Hebron: Lakini huyo mtumishi asili yake ni MUNGU au ni shetani kabisa?
Isaya: Asili yake ni shetani.
Nabii Hebron: Kwa hiyo na wewe katika kufufua misukule ulikuwa unawasaidia?
Isaya: Ndiyo
Nabii Hebron: BWANA YESU asifiwe. Ndugu mtazamaji, dunia imekwisha, lakini usiogope maana huyu ambaye nanaongea naye ndiye alitumwa pia ili kwamba aniteke na mimi.
BWANA YESU asifiwe. Na unaweza kunieleza mikakati ya shetani kuhusu ulimwengu wa kanisa?
Isaya: Ndiyo
Nabii Hebron: Karibu, endelea.
Isaya: Mkakati ambao aliupanga yeye ni kuliharibu kanisa na kuharibu jina la MUNGU. Ndio maana akaamua kuteka wachungaji maana wapo wachungaji ambao waliitwa na YESU, YESU mwenyewe aliwatuma, lakini shetani aliwajaribu akawapitishia tama mbalimbali ambayo ingeweza kuwaangusha ili wamwache YESU, na alifanikiwa katika hilo, ndio maana wachungaji wengi sana wamepotea. Na itu kingine ambacho shetani alikuwa pia amekipanga ni kukamata kila fahamu ya mtu duniani, ateke fahamu yake, akaitiishe yeye. Kwa hiyo mtu anakuwa anafanya mambo ya ajabu, watu wanamuona anafanya mambo ya ajabu, lakini kwa kufuatilia zaidi ni fahamu yake imetekwa na shetani, na hatimaye wote waende kwake, wasiendi mbinguni ili siku ya mwisho katika adhabu ya moto awe naye.
Nabii Hebron: Unaweza kutueleza jinsi ulivyookolewa kutolewa kuzimu? Unaikumbuka hiyo siku ilikuwaje?
Isaya: Nakumbuka.
Nabii Hebron: Karibu, endelea.
Isaya: Nakumbuka hiyo siku ilikuwa ni siku ya sadaka, nilisimamia sadaka.
Nabii Hebron: Sadaka za wapi?
Isaya: Sadaka za kuzimu ambazo watu wa kuzimu walikuwa wakitolewa
Nabii Hebron: Ambazo hizo sadaka za kuzimu watu wanaotoa ni sadaka gani?
Isaya: Damu, ili waweze kumpelekea baba yao ambaye ni joka kuu mwenyewe. Nilikuwa nikisimamia hiyo kazi, na baada ya kumaliza tukawa tumekaa kama kwenye kikao; kuzimu nzima imekusanyika, majini yote yanayokaa kwenye bahari na yanayokaa kuzimu ambayo ndiyo mapepo; tukakusanyika wote. Nakumbuka ghafla tukasikia kama upepo mkali unavuma, nikaambiwa angalia ni kitu gani. Niliangalia juu, kwa kweli niliona kundi la watu weupe wamevaa nguo nyeupe, na mmoja amevaa nguo nyeupe naye anakuja kwa kasi sana. Halafu pembeni nikamuona Mtume na Nabii.
Nabii Hebron: Yupi:
Isaya: Hebron.
Nabii Hebron: Enhe.
Isaya: Walipofika mahali pale, kwa kweli hakuna mtu ambaye aliweza kustahimili ile hali iliyotokea.
Nabii Hebron: Nini kilitokea hawakustahimili?
Isaya: Ulikuja mwanga mkali, na nguvu za ajabu, yaani tuseme tetemeko. Lilikuwa tetemeko kali na sauti kali sana.
Nabii Hebron: Sauti inasemaje?
Isaya: Walikuwa kama wanakuja wakiwa wameandamana tuseme wanakuja wanataka kutetemesha kuzimu sasa. Baadhi ya watu walianza kukimbia, hata mimi pia nilikuwa nikikimbia lakini nilishindwa, Mtume na Nabii Hebron alinifuata tukawa tunakimbizana, kila nilipopita nay eye anapita huko huko mpaka mwisho ulinikamata.
Nabii Hebron: Enhe, baada ya kukamatwa nini kiliendelea?
Isaya: Nilivyokamatwa, nilinyanyuliwa, niliwekwa juu kabisa, halafu huku chini kukawa kunaendelea vita, lakini ile vita nikawa siwezi kuingilia tena. Ikawa ni kama nguvu zangu zimenyonywa, sina nguvu tena. Kukawa kuna watu wawili kati ya wale wailiokuwa wamevaa nguo nyeupe wakawa wamenishika.
Nabii Hebron: Unaweza kuwakumbuka hao watu wawili?
Isaya: Ndiyo
Nabii Hebron: Majina yao?
Isaya: Majina hapana
Nabii Hebron: Sura?
Isaya: Sura nazikumbuka
Nabii Hebron: Endelea tu.
Isaya: Nilivyokamatwa baada ya ile vita kuendelea Mtume na Nabii akaniambia njoo mwanangu. Sikuelewa kwa kweli, ila nikachukuliwa, nilishikiliwa nikajikuta tu tayari nipo duniani, na nikaona mtu amekuja akaniambia twende kwa wazazi wangu lakini bado hawakujua kama miaka ya nyuma walikuwa wanakaa na jini, mimi ndio nikaenda.
Nilipelekwa na mtu akiwa anaendesha gari, nikapelekwa mpaka nyumbani, lile jini lilikuwa linakaa nyumbani liliaga likasema linaenda kwa mama, kwa hiyo na mimi nilivyorudishwa lile jini likatoka nikarudishwa mimi nikiwa nadai nimetoka kwa mama, kwa hiyo wazazi wangu hawakuweza kujua ni kitu gani kilikuwa kinaendelea.
Nabii Hebron: Na kule kuzimu uliniambia katika cheo walichokuwa wamekupa kulikuwa na vitu walikuwa wamekupa kama vile ishara ya kifalme kama fimbo na vitu vingine. Unaweza elezea hiyo fimbo?
Isaya: Ndiyo
Nabii Hebron: Endelea
Isaya: Ile fimbo kazi yake ni kama ku-command (kuamrisha) watu.
Nabii Hebron: Ni fimbo ya nanma gani?
Isaya: Ni fimbo ya dhahabu.
Nabii Hebron: Ambayo ulipewa na joka kuu?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Na kwa nini joka kuu alikupa wewe? Kwa sababu wewe ulikuwa mtoto pekee?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Ukiwa mwenye nguvu!
Isaya: Ni kweli, ndiyo.
Nabii Hebron: Uliniambia wazazi wako walihangaika na hata aliyekuleta kwenye maombi mpaka Arusha walikwenda sehemu mbalimbali kwenye makanisa, ila usitaje jina, labda mikoa uliyokwenda. Kwa nini walikuwa wanakufukuza?
Isaya: Ni kwa sababu mimi ni mkuu wao. Na siku zote, kawaida tuseme ni askari; askari hawezi kumshika kichwa kamanda. Ndicho walichokuwa wanakifanya, kwa hiyo wakkiniona wanazuiwa wanaambiwa msimguse huyo mtoto kwa sababu na wao walikuwa wakitii kwa kujua wakinigusa adhabu yao ni kubwa na wangeweza kudhalilika.
Nabii Hebron: BWANA YESU asifiwe. Ndugu mtazamaji, hali halisi ndivyo ilivyo, lakini usiogope. Huyu ni mwanadamu ambaye alikuwa na cheo cha tatu, kwa hiyo wachawi wote katika dunia nzima, majini yote, sijui wanajimu, hakuna ambaye anamkuta huyu, na ili mtu yeyote apate cheo chochote kwa shetani lazima anapitia hapa. Iwe ni rais, iwe ni mawaziri, iwe ni wabunge, na sehemu mbalimbali wafanyabiashara na mtandao wote wa freemason ulikuwa chini ya kijana huyu. Sasa hivi ni mwana wa YESU anazidi kutuelezea. Karibu tuendelee.
Isaya: Asante. Lengo labda niseme mpaka sasa hivi ningeendelea shetani alichokuwa amekipanga mbele yangu ningeendelea kuwa bado na zile nguvu zangu lakini zingezidi zaidi na hatimaye nilikuwa nakuwa shetani na mimi.
Nabii Hebron: Kabisa?
Isaya: Kabisa kabisa.
Nabii Hebron: Unaweza nielezea sura ya shetani ilivyo?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Ikoje? Maana watu wanasikia shetani wanachora mapembe, wanachora nini, elezea kwa kifupi tu.
Isaya: Shetani sura yake ipo kwa kawaida. Lakini mwenyewe amepaka kitu kama wanja, nao binadamu nashangaa nao pia wanatumia.
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Amepaka wanja jicho lake moja la upande wa kulia na pia ana mabawa mawili na ana kucha yake moja mkono wa kushoto.
Nabii Hebron: Ni kama mwanadamu kabisa?
Isaya: Ni kama mwanadamu, lakini ana mkia yeye pia.
Nabii Hebron: Ana mkia?
Isaya: Ndiyo
Nabii Hebron: Na joka kuu sura yake? Waweza kuielezea?
Isaya: Ndiyo
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Joka kuu ana sura, lakini ile sura yake yeye ukiangalia kama binadamu kwenye kichwa ana pembe na ana pua kubwa lakini kwenye pua yake kuna kitu amevaa kama bangili tuseme, kachomeka kwenye pua, na yuko kama nyoka, nyoka ambaye ni mkubwa sana. Yule nyoka ana vitu vilivyochongoka chongoka juu yake na ana vichwa saba.
Nabii Hebron: Ana vichwa saba?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Sasa wewe ulipokuwa kule chini, joka kuu si alikuwa anakuita mtoto wake?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Ulikuwa humuogopi?
Isaya: Hapana, kwa sababu ndiyo mazingira niliyokuwa nimekulia.
Nabii Hebron: Na maisha ya lusifa na joka kuu huko kuzimu yakoje?
Isaya: Lusifa anakaa sehemu yake, labda tuseme ni kama duniani, maisha ya duniani yalivyo, ndiyo maisha ya lusifa anayokaa lakini maisha ya joka kuu yeye anakaa zile sehemu za adhabu. Kuna sehemu kama kuna moto, amefungiwa kwenye ule moto. Hawezi kutoka pale. Na katika huo moto pembeni kuna sadaka zilizotolewa damu zimetawala katika ile sehemu.
Nabii Hebron: Unaikumbuka siku joka kuu alipofungwa?
Isaya: Nakumbuka.
Nabii Hebron: Ilikuwaje, na ni mtumishi gani alitumika kumfunga?
Isaya: Ni ghafla, tulishtukia ila tukapata habari kwamba anatafutwa na anatakiwa akamatwe.
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Alihama akatoka mahali alipokuwa anakaa, hakuaga anakwenda wapi wala hakutueleza ila tukastukia hayupo. Na mtumishi ambaye alichaguliwa katika kusuka kumkamata joka kuu ni mtumishi Hebron. Baada ya muda tuseme ni kama majira ya saa sita usiku, tukapata habari kwamba amekamatwa na amefungwa, akatupiwa hiyo sehemu ambayo anakaa mpaka sasa hivi ambayo ni sehemu kama ya adhabu, amefungwa fungwa hawezi kutoka.
Nabii Hebron: Na baada ya kufungwa, miaka 1,000 (elfu moja) mlitangaziwa imeanza?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Sasa ni YESU anatawala. Sasa ni kwa nini wanamtafuta Nabii Hebron?
Isaya: Wanajua wakishampata hakuna kitu tena kitakaa sawa hapa duniani. Wanaamini wao kwa imani yao, wanajua wakimpata wanaweza kutoa adhabu kali sana duniani kwa wale ambao wailkuwa wamemfuata YESU.
Nabii Hebron: Na jambo linguine, walijuaje mimi nimeitwa na YESU? kuzimu na joka kuu na wewe ukiwa huko ulijuaje na leo hii mpaka uko kwenye mikono yangu kimwili hapa tumeshikana?
Isaya: Nakumbuka ilikuwa ni majira ya mchana, tukapata habari kwamba YESU anakuja siku ya leo, lakini hatakuja mahali ambapo sisi tupo. Anakuja duniani, na anakuja kwa mfano wa sauti, anakuja kumfuata mtumishi ambaye yupo anafanya kazi Serengeti.
Nabii Hebron: Enhe, Serengeti kabisa?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Tukapata habari kwamba anavyomfuata anaenda kumpa maagizo afanye kazi yake. Kwa hiyo tangu siku ile ilinuka vita lakini hakuna kitu iliwezekana.
Nabii Hebron: Na mimi ndugu mtazamaji nashangaa YESU aliniita nikiwa Serengeti, sasa nashangaa na nyie mlijua! Ninyi mlijuaje? Mna vyombo vya kujua?
Isaya: Wana kama upeo wa jicho. Hilo jicho kwa sisi watatu ambapo mimi pia nilikuwwa wa tatu kati ya hao, tulikuwa tuna jicho moja ambalo linakaa kwenye paji la uso. Badala ya macho haya mawili ya kawaida kutumika kuangalia tu kuzimu, hilo jicho linaweza kuangalia duniani likajua kila kitu kinakwendaje na inatakiwa ifanywe nini ili waweze kusababisha kitu Fulani huku ulimwenguni.
Nabii Hebron: Baada ya kusikia sauti inaita mtumishi akiwa Serengeti, nilivyoipokea mliniona?
Isaya: Ndiyo
Nabii Hebron: Na baada ya Hapo kuendelea kwa hiyo mkaanza vita kupambana na mimi. Je, hakukuwa na watumishi wengine, ambapo mimi nilikuwa mchanga hata kiroho. Hao wengine hamkuweza kuhangaika nao mpaka mimi tu?
Isaya: Baadhi tuliweza, ila yuko mmoja kabla yako ambaye alikuwa anaitwa Moses Kulola ambaye ndio alikuwa akitafuta mtoto wa kiroho badala yake kwa sababu alishakuwa amezeeka amechoka. Na alikuwa akiomba muda mrefu sana ampate huyo mtu. Tulivyokuwa kila tukijaribu tukitamka jina lake, anayetamka jina lake ni kifo kinamhusu hapohapo.
Nabii Hebron: Mkitamka Moses Kulola?
Isaya: Ndiyo
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Tunakumbuka pia hiyo siku wewe ulienda ulifika kanisani kwake, na ulipelekwa na mtoto wake.
Nabii Hebron: Enhe.. Ni Dar es Salaam kweli nilikwenda. Mlijua nimeenda nyumbani kwake?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Ni ajabu! Enhe..
Isaya: Ulifika hapo kwake akakubariki. Kwanza alifurahi sana, akapiga magoti akasema asante MUNGU kwa kuniletea nilichokuwa nakiomba.
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Na sauti ilisikika ikasema “huyo ndiye uliyekuwa unamtafuta kwa muda, umekabidhiwa sasa”. Kwa sababu muda wake ulikuwa umeisha, amezeeka sana na kwa sasa yeye yuko mbinguni.
Nabii Hebron: Mnajua kabisa yuko mbinguni?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Enhe…
Isaya: Ile siku ulimbariki, na akafurahi sana, na yeye pia akakubariki. Alikufa, na kule takafikiri itakuwa ni njia nyepesi zaidi kwa kuonana na wewe na kukukamata lakini tulivyokuwa tukijaribu tunashindwa, tunakumbuka tukijaribu, tukisema tunajaribu kwenda, kitu tuliyokuwa tukikutana nayo pale kwa kweli ni hatari sana.
Nabii Hebron: Ni ninimlikuwa mnakutana nacho? Elezea tu.
Isaya: Tunakutana na jeshi ambalo limesimama, tuseme ni jeshi la malaika, halafu tunakutana na moto wa hatari na majabali. Kwa hiyo tulikuwa kila anayejaribu, anayejifanya mbishi, yeyote anayesogea vinamhusu kama sio moto, ni jabali au adhabu ya malaika.
Nabii Hebron: Ninashangaa, kweli nilikwenda kwa Moses Kulola, na mimi aliniambia ndugu msikilizaji, sijawahi kubarikiwa, wewe ndiye unanibariki kwa sababu wote walikuwa wamemwacha YESU na huyu anashuhudia kabisa. Kwa hiyo mtoto wake na wewe ulimwona?
Isaya: Ndiyo
Nabii Hebron: Unaweza kumbuka jina lake?
Isaya: Hapana, jina sikumbuki.
Nabii Hebron: Nilikuwa na mtoto wake anaitwa Willy, ndiye aliyenipokea nikiwa na gari, pamoja na watumishi niliokuwa nao. BWANA YESU asifiwe. Huo ndio ukweli wa hali halisi na mambo yalivyo. Na sasa hivi, kwa kiwango mlichokuwa mmefikia, kwa sababu tunasikia injili ulaya, injili dunia nzima, mara Afrika Magharibi, hizi injili zina namna gani? Ni za YESU au ni za shetani?
Isaya: Hizi injili ni za shetani; kwa kweli ni za shetani, na shetani aliamua baada ya kuona hawezi katika vitabu vya Biblia, akaamua kuingiza ya kwake kwenye simu, tuseme ni mtandao wa Internet, na ile biblia ambaye anasoma kwenye ile simu, roho za shetani zinamuingia na yeye pasipo yeye mwenyewe kuelewa. Kwa hiyo hata kama yupo kwa mtumishi wa kweli anapokuwa anaitumia ile biblia kuisoma bado hatapata faida, wala hataweza kufanya chochote na kufanikiwa katika maisha yake kwa sababu bado anatumia ulimwengu wa shetani.
Nabii Hebron: Na baada ya marehemu Moses Kulola kuondoka nikabaki mimi, nyie mliona mimi ni mtoto mtaniweza?
Isaya: Ndiyo
Nabii Hebron: Sasa dunia nzima hakukuwa na watumishi wengine mpaka mhangaike na mimi tu?
Isaya: Kwa kweli kulikuwepo na watumishi lakini ni wale baadhi yao ambao waliitwa na YESU, MUNGU mwenyewe aliwachagua wafanye kazi yake, ambao walikwenda kinyume wakafanikiwa kukamatwa na shetani. Tulikuwa tunawatumikisha wenyewe na walikuwa hawana uwezo wa kutufanya chochote, hata hatima za mwisho hawawezi kukamata watu wakawaweke kwenye mstari wa MUNGU mwenyewe, ila wewe ndiye uliyekuwa unaweza kukamata watu na kuupeleka ulimwengu mzima kwa MUNGU. Na tunakumbuka pia siku ambayo YESU alikuwa anakuagiza, alikuambia na madhabahu yangu naomba uiite MADHABAHU YA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE ili mataifa yote yaje kwangu.
Nabii Hebron: Na hilo mlilisikia pia?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Sasa, kwa sasa hivi kwa nyakati mlizokuwa kuzimu mnajua hizi ni nyakati za mwisho ni mikakati gani wanahangaika na kuhusu mataifa yote ili wasimwone MUNGU?
Isaya: Ni Kupotosha.
Nabii Hebron: Kwa njia gani?
Isaya: Kama tuseme kuwakamata katika uzinzi, wizi, ulevi, na hata katika mambo mbalimbali ambayo wao wangeweza kwenda kinyume na amri za MUNGU.
Nabii Hebron: Na jambo lingine ambalo nahitaji kukuuliza kwa ajili ya faida ya wasikilizaji na watazamaji, maana mimi nilikuwa nayajua yote tangu nilivyokuwa nakutoa juko chini sawa sawa na YESU alivyoniagiza. Sasa hivi baada ya kutolewa maana joka kuu amekwisha kufungwa, katika nchi ya Tanzania, inaenda kuwa nini?
Isaya: Nchi ya Tanzania kwa kweli inakwenda kuwa nchi kubwa na ni nchi ambayo watu wote watabadilika na kumfuata MUNGU hapo baadaye na itakuwa ni Edeni ya MUNGU mwenyewe.
Nabii Hebron: Kupitia wapi? Nani atasababisha itokee hivyo? Atatumiwa mwanadamu gani?
Isaya: Mtume na Nabii Hebron mwenyewe.
Nabii Hebron: BWANA YESU asifiwe, na hebu nieleze wale ma-rais, mawaziri ambao ulikuwa unawapa vyeo, wabunge, wafanyabiashara ni namna gani ulikuwa unawapa vyeo? Maana kuna wachungaji nasikia wanataka uaskofu wanapewa vyeo, na makanisa mengine kwa nini wanaweka bendera, na watumishi kwa nini wanaweka bendera kwenye magari yao?
Isaya: Kwanza kabisa, ile bendera inayowekwa kweye gari au kwenye madhabahu sharti ambalo walipewa zilitakiwa ziwekwe bendera nne, zisizidi. Na kwenye magari waliambiwa waweke bendera moja.
Nabii Hebron: Ya nini?
Isaya: Ya nchi yoyote, ambayo inaashiria kulingana na vyeo vyao mchungaji huyu labda cheo chake yeye ambapo mimi ndiye nilikuwa natoa hicho cheo, labda anapewa cheo cha yeye kuhangaika na nchi Fulani kama mfano tuseme ni Kenya, anaweka bendera ya Kenya kwenye gari yake na kama kuna mtumishi mkubwa kidogo, ambaye yeye kwa juhudi zake alizofanya nikimpa cheo.
Nabii Hebron: Kutoka kwa shetani?
Isaya: Ndiyo, anapewa cheo labda cha kukamata nchi nne, ndio maana unakuta mtu kwenye madhabahu ameweka bendera labda tuseme ya America, Tanzania, Sweden na North America, hicho ndio kinakuwa cheo chake yeye.
Nabii Hebron: Kuzikamata hizo nchi?
Isaya: Ndiyo. Ni kuzikamata hizo nchi na kuzishusha kwa vitu mbalimbali kama vile uchumi, amani, hata watu wa ile nchi kupata shida, yaani mateso.
Nabii Hebron: Chanzo ni hizo bendera?
Isaya: Ndiyo
Nabii Hebron: Sasa nikuulize swali, Je, madhabahu ya MUNGU aliye hai inaruhusiwa kuwekwa bendera?
Isaya: Hapana, hapana.
Nabii Hebron: Ni kwa nini wengine wanaweka bendera hata ishirini za mikoa mbalimbali kanisani na mwingine unakuwa ni mtumishi anajiwekea bendera yake, anabuni mwenyewe. Hiyo kubuni bendera yake mwenyewe ina maana gani?
Isaya: Anavyobuni ile bendera yake, ina maana yeye kulw kuzimu ameshapewa cheo na shetani cha kutengeneza serikali yake mwenyewe.
Nabii Hebron: Ahaa.. Mnasikia ndugu wasikilizaji? Enhe..
Isaya: Ambayo labda tuseme watumishi ambao watakuwa katika kanisa lake na waumini watakaokuwa katika kanisa lake, kwa hiyo wanavyokuwa wengi na wengi wanavyozidi ndivyo anavyokuja kutengeneza serikali yao ambayo labda kwa jina la mtumishi yeyote na ile serikali ataiita kwa jina lake.
Nabii Hebron: Na hiyo serikali na wale waumini mwisho wake ni mbonguni au ni kuzimu wanarudi?
Isaya: Ni kuzimu.
Nabii Hebron: Na mbona wengi wanasema ni watumishi wa YESU na wana hizo bendera za kwao, ni bendera za namna gani? Ndugu watazamaji na wasikilizaji wangependa kuelewa.
Isaya: Hizo bendera tusema zina namna yake ambayo kama mtumishi yupo Tanzania, anakuwa lazima aweke ile bendera ya Tanzania, kwa sababu yeye anahusika na nchi ya Tanzania na mahali anapoishi. Kama ni mkoa fulani na anaishi katika mkoa fulani, tuseme katika kata fulani, anapewa mamlaka ya kukamata ile kata, nchi na huo mkoa. Na hatimaye huweza kuunda serikali yake kwa haraka sana.
Nabii Hebron: Kwa hiyo ndiyo maana unashangaa makanisa yanakua ki-ajabu ajabu?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Mtumishi anaibuka mara moja, wanasema ni MUNGU, ana ma-helikopta, na hammer na ndege, yote hayo ni wewe ulikuwa unawakabidhi bwana mkubwa?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Sasa hivi uko kwa YESU. Unajisikiaje? Unatamani tena kurudi huko?
Isaya: Hapana kwa kweli.
Nabii Hebron: Maisha ya YESU na maisha ya huko unayaonaje?
Isaya: Maisha ya YESU ni mazuri zaidi kuliko ya huko.
Nabii Hebron: Kwa nini?
Isaya: Kwa sababu, kama ule usemi ambao umeandikwa, au tuseme ni usemi ambao watu wanapenda kusema, kwa YESU kuna kila kitu. Kuzimu vipo baadhi, na vingine hakuna. Kwa YESU kuna ushindi, kwa YESU kuna vitu mbalimbali, hata mwenye shida anapopiga goti na kumlilia YESU ile shida yake hufanyika na kutegemezwa hapo hapo. Ila ni imani yake inatakiwa.
Nabii Hebron: Haya, sasa unawaambiaje ndugu wasikilizaji na watazamaji kuhusu habari ya kuzimu? Maana naona kuzimu watu wanakula damu za watu.
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Na kila mtu ambaye amepata cheo kwa njia za uchawi amelishwa nyama za watu?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Na wanatumia vichwa vya watu kama sahani!
Isaya: Ni kweli.
Nabii Hebron: Sasa huku duniani mbona wanatamba wana pesa, wanafufua misukule watumishi; kwa hiyo wote hawa wakula damu na nyama za watu?
Isaya:Ndiyo.
Nabii Hebron: Na nini zaidi, hebu elezea.
Isaya: Kwanza, wanakuwa wanakunywa damu, ni hatua ya kwanza ambayo wanaita ni kama muhuri.
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Na kujulikana katika serikali ya shetani. Wanakunywa damu halafu hatua ya pili baada ya kupewa damu wanaangaliwa; je, wanaweza? Hatua ya pili inakuwa ni kutafuna nyama za watu.
Nabii Hebron: Enhe….
Isaya: Ambayo mtu anashauriwa labda ndugu yako umlete mama yako, baba yako, kaka yako au dada yako.
Nabii Hebron: Umtoe kafara?
Isaya: Umtoe kafara ndiyo, hatua ya tatu baada ya kula nyama, kichwa cha yule mtu ambaye anakuwa anatolewa sadaka huwa hawakikati, ila anapopelekwa huyo mtu mahali pale pa kutolea “sacrifice” anakuwa kuna chombo kinatumika kumpiga kichwa, wakimpiga katika kichwa, ikishuka kile kitu kinachotumika kumpiga kichwani inavyotolewa na uhai wake ndivyo unavyotolewa. Kwa hiyo kile kitu kinakuwa kinatumika kwa “style” (staili) hiyo halafu kichwa kinakatwa kinawekwa pembeni, kiwili wili ndio kinachobakia na ndio wanachokitafuna, na mtu wa kwanza anakuwa ni yule ambaye anataka kuhesabiwa katika serikali ya shetani, wengine wanafuata nyuma ambao ni watumishi wote na wanakuwa wanapewa hatua nyingine ya kuua hata ndege nzima.
Nabii Hebron: Kuangusha chini?
Isaya: Kuiangusha
Nabii Hebron: Wewe umeshawahi kuangusha ndege?
Isaya: Hapana.
Nabii Hebron: Meli?
Isaya: Hapana.
Nabii Hebron: Wewe ulikuwa unatoa maelekezo tu?
Isaya: Mimi natoa maelekezo.
Nabii Hebron: Unakumbuka maelekezo ulishatoa ya kuangusha vitu?
Isaya: Ndiyo ninakumbuka.
Nabii Hebron: Hebu nielezee.
Isaya: Baadhi nakumbuka.
Nabii Hebron: Baadhi tuu!..
Isaya:Ndiyo; kama ya ndege. Nilikuwa nasema mtu ambaye anataka cheo fulani, labda urais, uwaziri au ubunge, kwa sababu sisi tulikuwa hatutuo vyeo kwa madiwani au wenyeviti wa serikali za mitaa.
Nabii Hebron: Mpaka vyeo vikubwa vikubwa?
Isaya: Vile vyeo vya kuwanzia ubunge na kuendelea mpaka urais ninamwambia nilikuwa namwambia kama ni ndege yenye ukubwa gani ambayo joka kuu mwenyewe anaweza akakubali sadaka ya yule mtu ili aweze kupata kile cheo anachokihitaji. Kama ni joka kuu labda anahitaji vitu vingi, anahitaji labda apoteze uchumi wa nchi.
Nabii Hebron: Nchi fulani?
Isaya: Nchi fulani, anakuwa anahusishwa katika zile ndege za cargo.
Nabii Hebron: Cargo?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Za mizigo.
Isaya: Kama tuseme KLM, anaambiwa aende airport (uwanja wa ndege), akaseme yeye anasafiri, aende ule muda ambao ile ndege itaruka, na akifika hapo kwenye uwanja, anaingia katika ile ndege kwenye kitu chochote, mahali popote, hata kwenye tairi.
Nabii Hebron: Kipepo?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Anaweka kitu hicho kwnye hiyo kitu, ni yeye mwenyewe atakapojisikia pa kuweka.
Nabii Hebron: Enhe…
Isaya: Anapoweka hiyo kitu kipepo, watu wanamwona anapanda hiyo ndege, lakini yeye mwenyewe hayupo pale, anakuwa anavyoweka kile kitu akipanda ndege yake ndiyo maana unakuta anasema labda anatoka Dar (Dar es Salaam) anaenda Arusha, halafu anarudi siku hiyo hiyo.
Nabii Hebron: Enhe…
Isaya:Ile ndege itakavyoruka baada ya kufika umbali fulani inaanguka, inavyoanguka kunakuwa labda kuna vitu vya nchi fulani ambavyo vina thamani sana kwa watu, anapokuwa ameangusha vile vitu, kama joka kuu ataridhika na ile sadaka yake, anapewa cheo chake.
Nabii Hebron: Unaweza kukumbuka matukio ambayo ndege zimeanguka?
Isaya: Naweza kukumbuka.
Nabii Hebron: Nitajie machache.
Isaya: Ethiopian Airways, na ndege kutoka Asia kwenda Malaysia.
Nabii Hebron: Ilikuwaje? Na mbona ndege inatafutwa hapa duniani mpaka sasa hivi haijapatikana?
Isaya: Ile ndege ilipelekwa kabisa kuzimu, haikupitia pale kwenye bahari, ilipotea kabisa kabisa.
Nabii Hebron: Kuzimu kabisa imefika kwa hiyo?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Na njia iliyopitishwa maana walitumia vyombo vingi kuangalia hawajaipata. Ni kwa nini hawajaipata?
Isaya: Ni kwa sababu njia ambayo wao binafsi wanatumia ni njia ya kipepo.
Nabii Hebron: Kutafuta kipepo?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Kwa hiyo walitakiwa watafute kwa njia ya Ki-MUNGU.
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Kwa hiyo ndege ile ipo kuzimu kabisa?
Isaya: Ipo kuzimu.
Nabii Hebron: Na wale watu wote?
Isaya: Wale watu wote walichukuliwa wakatolewa sadaka.
Nabii Hebron: Enhe…
Isaya: Ile ndege iliyeyushwa kimazingara, haikuonekana kuzimu tena, sijui ilifikia nchi gani.
Nabii Hebron: Na ndege gani nyingine tena unaikumbuka?
Isaya: Kwa kweli sikumbuki nyingine.
Nabii Hebron: BWANA YESU asifiwe. Na habari ya vita, tumesikia nchi nyingi zina vita.
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Je, na hapo ulikuwa unahusika?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Enhe… Kama nchi gani na nchi gani?
Isaya: Kama China, Syria, America, Saudi Arabia na Sudan.
Nabii Hebron: Na ulikuwa ni namna gani unahusika maana sasa hivi haupo tena huko?
Isaya: Ni kutengeneza faraka, unatengeneza faraka kama labda ni America na Syria, unaanzisha vurugu labda Syria wanarusha bomu nchi fulani, ile nchi unawaongezea hasira.
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Wanapopatwa na hasira, wanavyorusha tena kule inakuwa ni vurugu imeshatokea tayari.
Nabii Hebron: Kwa hiyo vita inavyotokea, ninyi mnakuwa mnapata faida gani?
Isaya: Wao walikuwa wakichukua damu.
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Wanachukua damu, wanachukua na watu wenyewe na ndio maana unakuta labda katika ajali inayotokea, unasikia wengine hawakuonekana, na wengine walionekana. Kwa hiyo baadhi ambao unakuta damu zao zinaendana na damu ambayo joka kuu na lusifa mwenyewe anazitaka, walikuwa wakichukuliwa kabisakabisa.
Nabii Hebron: Na nikuulize, wewe ulishawahi kula nyama ya mtu?
Isaya: Hapana.
Nabii Hebron: Damu ya mtu?
Isaya: Hapana.
Nabii Hebron: Kwa nini hukula?
Isaya: Ni MUNGU tu mwenyewe tuseme.
Nabii Hebron: Na ingali ulikuwa na cheo kikubwa huko chini?
Isaya: Ndio maana nikasema ni mipango ya MUNGU mwenyewe, kwa sababu niikuwa nikisimamia damu ya mtu labda inatakiwa itolewe, nasimamia kuanzia mwanzo mpaka inapokwisha, lakini mimi mwenyewe hapana. Hata lusifa alipokuwa anajaribu kuniambia chukua, joka kuu alikuwa akimkataza mwenyewe anamwambia hapana, acha usimpe.
Nabii Hebron: BWANA YESU asifiwe. Ndugu watazamaji na watoto wa MUNGU mnaompenda YESU, mnaotazamia kwenda mbinguni, nitamwachia mwana wa MUNGU aliyetolewa kuzimu, kwa jina anaitwa Isaya sio Max tena, aelezee hayo mengine yeye mwenyewe, karibu.
Isaya: Asante, labda ningependa kuwaeleza kuhusu shetani mwenyewe. Shetani kazi yake kubwa ambayo yeye mpaka sasa hivi anafuatilia katika ulimwengu ni kupata vitu vingi kama vile kupotosha watu kwenda kuzimu kumfuata yeye na sio kufuata njia ya MUNGU. Na kuendelea kuingiza roho zake mwenyewe kama vile uzinzi, wizi; majambazi wamezidi duniani, nab ado anachoendelea kufanya yeye ni kupambana. Shetani mwenyewe huwa hachoki na hakati tamaa siku zote, kwa hiyo kitu ambacho shetani anafanya, anataka akamate ulimwengu, kwa hiyo wana wa MUNGU mnatakiwa muwe makini sana na hilo kwa sababu shetani akikukosa kwenye uzinzi, atakukamata kwenye wizi, akikukosa kwenye wizi, atakukamata katika vurugu mbalimbali kama tuseme casino anweza akakukamata hata hapo. Akikukosa hapo, atakukamatia kwenye vitu vyake vingine, ambavyo hata mimi sasa hivi baadhi sivikumbuki. Kwa hiyo wana wa MUNGU mnatakiwa muwe makini sana na shetani, kwa sababu shetani hakati tamaa. Unaweza ukamfamfanya shetani hiki sasa hivi ukamkataa, atakuacha na wewe utasema shetani ameniacha ila mwenzako anakutafutia ‘timing’ akukamatie mahali gani. Anaweza akakukosa hapo ambapo wewe umepasema, akaja akakukamata kwenye kitu kingine ambacho ni zaidi ya kile cha kwanza ukatenda dhambi na kumuudhi MUNGU zaidi ya pale. Na labda ningependa kuwaambia kuzimu kitu inaendelea, hata wale wenzetu ambao wanafanyiwa ibada za wafu. Ile ibada husimamiwa na mapepo mbalimbali wanasimama pale. Hata katika lile jeneza hawi tena mtu, anatolewa roho yenyewe, pale wanaacha tu ligogo. Mtu mwenyewe anakuwa ameshapelekwa kuzimu. Na hata mnavyokuwa mnaomba, mnasali, ile kitu hakuna tena kwa sababu hata Biblia inasema MUNGU husikiliza maombi ya mtu akiwa hai, akishakufa hana kazi tena. Kwa hiyo, hata mkimuombea na kumfanyia ibada yoyote inakuwa ni kazi bure.
Nabii Hebron: Na ningekuuliza kwanza, maana niliposhuka niliona marais wako kule kuzimu na nikakumbuka wanazikwa kwa ibada nyingi sana, waheshimiwa kwa ajili ya mali zao, watu wanalia miaka na miaka, ila usitaje majina. Mimi niliona toka mwaka 1949 mpaka mwaka 2013, nafikiri hakuna rais aliyekufa yuko mbinguni. Je ni uwongo hayo ninayoyasema?
Isaya: Ni kweli. Ni kweli kabisa unachokizungumza.
Nabii Hebron: Hebu waeleze wanafanya nini huku chini sasa.
Isaya: Kama kazi yao ikishaisha duniani, zile roho MUNGU hazipokei mbinguni, kwa hiyo MUNGU anamwacha kwa sababu shetani anakuwa ameshamnyanyulia bango kabla ya kifo chake. Na MUNGU hawezi kuingilia kati, kwa hiyo anaacha ile maiti inabebwa, inapelekwa kuzimu na adhabu anapata kuzimu kwa sababu muda wake umeshakwisha. Haendelei tena kuishi kama kawaida, ila anapata tu adhabu.
Nabii Hebron: Adhabu gani labda?
Isaya:Kutumikishwa labda kupika vyakula.
Nabii Hebron: Kwa hiyo ni wapishi huko chini?
Isaya: Ndiyo. Kuwekwa kwenye moto labda,.
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Adhabu za kuwekwa kwenye moto, kupigwa, kubebeshwa mizigo mbalimbali.
Nabii Hebron: Enhe.
Isaya: Na vitu vingi vingi ambavyo nimeshavisahau.
Nabii Hebron: Ndiyo vibarua?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Wewe huko si ulikuwa ni kamanda?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Na mimi walikuwa wananiita majina gani nikiingia huko?
Isaya: Jina lako la kwanza walikuwa wnakuita mfalme, jina lako la pili walikuwa wanakuita mkuu, na jina lako la tatu walikuwa wanakuita kamatakamata.
Nabii Hebron: Kamata kamata?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Na jambo linguine nitakuuliza, unasema wewe ulikuwa ni mpokeaji wa sadaka mkuu?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Hizi za watu wote ambao wanaenda kwa wachawi, washirikina, makanisa ya kipepo?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Zile sadaka bila wewe kuzipokea zilikuwa hazipokelewi?
Isaya: Hazipokelewi kabisa. Na hata kama mtu anataka cheo fulani, akija kwangu kama labda ni mara yake ya kwanza akidharau, nikishamwambia hapana; hatarudi tena duniani. Hiyo ndio inakuwa kifo chake siku hiyo hiyo. Wanamuua wanamfanya yeye ni sadaka.
Nabii Hebron: Na hii habari ya muhuri, ni ya nini mlikuwa mnautumia?
Isaya: Muhuri?
Nabii Hebron: Huu muhuri wenu una kazi gani?
Isaya: Kazi yake ule muhuri ni kuukamata ulimwengu. Ndio maana hata katika ule muhuri wakaweka namba zao.
Nabii Hebron: Wakaweka namba ngapi?
Isaya: Ni mia sita sitini na sita (666).
Nabii Hebron: Enhe…
Isaya: Ule muhuri kuna mapepo ambayo yanatumwa yanatembea duniani, kwenye nyumba. Mida yao ni usiku saa nane, wanapiga kama kwenye nyumba kuna watu watano, wanapigwa wote muhuri, wakienda kwingine tena wanapiga muhuri, kwa hiyo inakuwa ni ulimwengu wote ameshakamata shetani mwenyewe. Kwa hiyo wale wote ambao wana zile alama za mia sita sitini na sita (666) ambazo zinapigwa kwenye paji la uso wanakuwa ni kundi la shetani tayari.
Nabii Hebron: Ok. Jambo linguine japo ndugu mtazamaji utaendelea kufuatilia vipindi vingine, mambo ni mengi; hebu tueleze namna ambavyo mlikuwa mnaweza kuitikisa nchi ya Tanzania na nchi nyinginezo. Na kama sasa hivi mnaweza kuitikisa tena nchi ya Tanzania.
Isaya: Kwanza kwa kweli kabisa Tanzania hawaiwezi kwa kitu chochote. Na hata wale ambao walikuwa ambao wakigombea labda urais, ubunge, uwaziri kwa njia ya kipepo hawawezi kufanikiwa tena. Hatima za mwisho wataanguka tu. Atatoka kwa MUNGU rais ambaye ataongoza Tanzania na mawaziri na wabunge ambao wataongoza Tanzania.
Nabii Hebron: Kwa nini? Ni nini imesababisha?
Isaya: Ni mpango tu wa MUNGU kupitia chombo chake ambaye ni binadamu ambaye ni Mtume na Nabii Hebron peke yake.
Nabii Hebron: Na jambo linguine, ni kwa nini watumishi wote walikushindwa? Maana uliniambia mwanadamu ni wewe tu uliyeniweza. Ni kwa nini?
Isaya: Kwanza walikuwa wanajua mimi nina kitu gani kizito, ambacho hata wao binafsi hawawezi kukistahimili wala kukitoa katika mwili wangu. Walishajua kwamba mimi mambo yangu ni mazito zaidi, na hawajawahi kuona kitu kama kile hapa duniani. Nayo pia ilikuwa inachangia katika wao kuogopa kunigusa wala kuniombea, japokuwa walikuwa wakiogopa baba yao lusifa na wakijua mimi ni nani yao.
Nabii Hebron: Sasa kwani Nabii Hebron Hebron ana nini tofauti na wenzake hao wengine?
Isaya: Nabii Hebron yeye, kwanza ameitwa kabisa kabisa, na alikubali ule wito wa MUNGU ndani yake. Hakwenda kinyume a ile amri ambayo MUNGU mwenyewe alimpa azifuate. Lakini wachungaji wengine walifuata tamaa, walitii tamaa, wakafuata mambo ya uzinzi, hata wachungaji wanazini na waumini na mambo mbalimbali, hata watumishi, manabii wameenda kinyume na amri za MUNGU ndiyo maana.
Nabii Hebron: Na jambo lingine nikuulize, unakumbuka jinsi ulivyoletwa kanisani?
Isaya: Ninakumbuka.
Nabii Hebron: Enhe… Na unakumbuka ahadi uliyopewa ukifanikiwa kunikamata mimi?
Isaya:Ninakumbuka ndiyo.
Nabii Hebron: Enhe, hebu elezea ndugu watazamaji.
Isaya: Ahadi ambayo nilikuwa nimepewa nikiweza kumkamata Mtume na Nabii Hebron, nitapewa kile cheo cha kuwa shetani kabisa kabisa.
Nabii Hebron: Na shetani angepewa kipi ungechukua nafasi yake?
Isaya: Shetani ningechukua nafasi yake ambaye ni lusifa.
Nabii Hebron: Enhe…
Isaya: Mini ngechukua nafasi yake, badala yake ningesimama mimi, na ningepewa mamlaka ya kutumikisha hata wale ambao ni wakubwa wa kule kuzimu, ambaye ni lusifa pamoja na joka kuu na msaidizi wao ambaye ni mama wa makahaba mkuu.
Nabii Hebron: Na katika serikali hiyo ya kuzimu uliyokuwepo, kwa hiyo lusifa alishanishindwa?
Isaya: Ni kweli, ndiyo.
Nabii Hebron: Wewe uliyekuwa msaidizi wake umeshashindwa?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: joka kuu naye amefungwa pingu.
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Nini kinaendelea sasa?
Isaya: Wamekaa tu kwa kweli, hawana cha kufanya.
Nabii Hebron: Kwa hiyo YESU anatawala sasa miaka elfu moja (1,000)?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Na kuhusu habari ya jina, maana nimeshangaa umeniambia ulisikia jina la kanisa liitwe kama nilivyoliita.
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Ni nini hili kanisa linaenda kufanya katika dunia?
Isaya: Hili kanisa kitu linakuja kufanya hapo baadaye, linakuja kufanikisha kuchukua watu wote na ulimwengu mzima warudi kwa YESU na kurudisha hata amani katika nchi na kufanya MUNGU awe karibu sana na watu na kufanya watu wasitende tena dhambi na wachukie sana dhambi na wamchukie shetani.
Nabii Hebron: Na jambo lingine mbona nimesikia kuwa dini kubwa za Kikristo mbalimbali na kuna wengine wanadamu wanajiita wao ni YESU; kwa sababu wewe ulikuwa ni kiongozi mkubwa, hayo yote unayajua.
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Ni kivipi hao?
Isaya: Wale watumishi ambao wanajiita wao ni ma-yesu, kwanza wanakuwa wamevalishwa ile sura ambayo waliiona katika picha ya yule Brian mwingereza; aliye-‘act’ ile ‘movie’, wakawa wanapewa ile sura na shetani ambaye ni lusifa mwenyewe, ambaye amesimama badala ya joka kuu. Wanakuwa wanapewa ile kitu, na wao wanakuwa muda ule hawako tena pale.
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Ila zinabaki ‘spirit’ (roho) zao ambazo zina nguvu za kipepo zaidi.
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Ndiyo. Kwa hiyo wanamuona amekuja amevaa nguo fulani; labda nguo fulani ambazo YESU alikuwa amevaa katika ile filamu aliyo-‘act’ Brian akiwa anapaa, anawaambia labda njooni mniguse. Wanapoenda kumshika, ndivyo wanavyoacha na vitu vyao pale, wanaondoka wenyewe, tuseme ni maboksi.
Nabii Hebron: Na jambo lingine,..
Isaya: Ndiyo,.
Nabii Hebron: Huoni wanadamu wanadanganywa maana yule ni mwanadamu? Picha ya YESU ndio imefanana na ile?
Isaya: Hapana.
Nabii Hebron: Si kitu tofauti kabisa?
Isaya: Ni kweli.
Nabii Hebron: Wewe YESU sura yake si unaijua?
Isaya: Naijua.
Nabii Hebron: Sasa kwanini wanadamu wanamwita huyo Brian YESU? Si unaona wanadamu wanavyoangamia? BWANA YESU ASIFIWE. Sasa mwana wa MUNGU Isaya, MUNGU akubariki sana.
Isaya: Amen.
Nabii Hebron: Na akuinue usiogope, usonge mbele.
Isaya: Amen.
Nabii Hebron: Mimi ndiye Baba yako wa kiroho, nakuambia hakuna kitu chochote kitakachokugusa.
Isaya: Amen.
Nabii Hebron: Wewe mwenyewe ulikuwa ni komandoo wa makomandoo wa huko. Kama ilivyo katika ulimwengu huu akina Osama, Hitler, huyu ni zaidi. Hata wapiganaji hawa wa nchi mbali mbali maarufu wanaotumia nguvu za giza, huyu ndiye alikuwa kiongozi wao. BWANA YESU asifiwe. Lakini msiogope, sasa ninawatia moyo, mumrejee BWANA YESU, sasa hivi ni wakati wa kumfuata YESU. Mambo yamekwisha kuharibika. Amenituma YESU kuwakomboa, mnaosikiliza; sikiliza mambo yameharibika. Leo hii hapa tupo na mtu ambaye ni nafasi ya tatu, ukisoma katika Biblia; joka kuu, lusifa, halafu ndio wa tatu. Ina maana wachawi wote dunia nzima ili wamfikie shetani au kupeleka sadaka zao walikuwa wanatoa hapa; ili apate cheo mtu alikuwa napeleka hapa. Sasa ametoka, nimtoa kuzimu sasa hakuna cha sadaka tena, nawaambia vyeo hakuna tena vya kipepo. Ni wakati wa YESU wa Nazareti kuinuliwa na kazi itaendelea mbele na mbele. Utukufu wa kanisa la mwisho umerejea. BWANA YESU asifiwe. Zaidi karibu katika kanisa la YESU BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, utafundishwa mengi, utabadilika. BWANA YESU asifiwe; kwa yule anayetaka.! Shetani ni mbaya. Leo umepata bahati ya kusikia mmoja wa wakuu. Tumesikia maajenti wametoka kuzimu, hao wote ni maajenti wa namna gani? Ni wadogo sana, si ndio?
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: Na hata kanisani kwangu mmewatuma wengi.
Isaya: Ni kweli.
Nabii Hebron: Enhe., wameishia wapi wale mlikuwa mnawatuma?
Isaya: Waliishia palepale, walivuliwa zile roho.
Nabii Hebron: Enhe..
Isaya: Na ndiyo ilikuwa mwisho wao kutumika na kuzimu.
Nabii Hebron: Nawatandika?!
Isaya: Ndiyo.
Nabii Hebron: BWNA YESU asifiwe. Hivyo nawasihi mrejee kwa YESU. Kwa unayesikiliza; sema BWANA YESU, naomba unisamehe, dhambi zangu zote, nilizozitenda kwa kujua au kutokujua. Namkataa shetani na kazi zake zote, na mambo yake yote, na serikali yake kuanzia sasa. Najipatanisha na BWANA YESU wa kweli. Namkataa shetani kwa nguvu na mamlaka ya jina la YESU. Nami nakuombea ndugu mtazamaji, BWANA YESU akufunike kwa damu yake, na malaika wake kwa jina la YESU akulinde. Na ujumbe huu toa dvd, wape na wengine na wengine, na kwenye youtube waeleze na wengine na wengine, na kwenye blog wengine na wengine utakujenga, utakuinua. Msidanganyike tena. MUNGU awabariki.
Karibuni Tanzania, karibuni katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. Amen.
NABII HEBRON.
[ad_2]