CHEO CHA ASKOFU KAMA KIONGOZI MKUU KATIKA KANISA LOLOTE CHEO HICHO CHA ASKOFU HAKIJATOKA KWA YESU BALI KIMETOLEWA NA SHETANI ILI KUMPINGA YESU!!

[ad_1]

v HUDUMA YA UASKOFU SIYO MOJAWAPO YA HUDUMA TANO ALIZOZIANZISHA YESU.

v HUDUMA YA CHEO CHA JINA LA ASKOFU NDIO AWE KIONGOZI WA KANISA NI MPANGO WA SHETANI SIYO MPANGO WA YESU ALIOACHA.

v HUDUMA YA UASKOFU NI HUDUMA YA NAMBA YA 6 KUTOKA KWA SHETANI ALITEKE.
Zaidi Soma Hapa!!!

Watu wote wa mataifa yote nawasalimu kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI aliye hai ndiye aliyelijenga kanisa linaloitwa kwa majina ya Kristo. Amenituma niwaeleze mataifa yote mumrejee yeye na mumrejee yeye sababu mamilioni ya watu wameshatekwa na shetani wala hawajielewi ni njia ipi wanayoiendea kivipi endelea kusoma makala haya ya Nabii Hebron. YESU WA NAZARETI alipokuwepo hapa ulimwenguni nawauliza swali je alilijenga kanisa lenye huduma ngapi? Jibu ni huduma tano tu ili wakamilishe kulijenga kanisa lake. Ukisoma Waefeso 4: 11-12 Naye aliwatoa wengine kuwa mitume na wengine kuwa manabii na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa Kristo ujengwe mpaka umeona kanisa alilolijenga katika msingi wa Manabii na Mitume, hii ina maana kuwa viongozi wa kanisa ni Mitume na Manabii, peke yake.
Na ukisoma katika Ufunuo 22: 18-19, inasema hivi “namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, mtu ye yote akiyaongeza, MUNGU atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu yeyote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, MUNGU atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”
Mpaka hapa unazidi kufunguka hata biblia inasema maneno yote ya injili ni ya kinabii wala haisemi ya kiaskofu. Na zaidi inasema mtu yeyote atakayeyaongeza maneno atahukumiwa, sasa angalia hapa hili neno Askofu wewe hauoni limezidi ni la sita, na YESU alichagua huduma tano tu katika kanisa. Je umeshawahi kujiuliza ilikuwaje mpaka mtu akaitwa Askofu, ndiye aliongoze kanisa? Najua ulimwengu hauelewi ila amenituma niwaonyeshe njia sahihi na atakayeifuata atapona roho yake atakaye kaza shingo yake iwe ngumu ajijue asahau habari ya mbinguni ajijue yeye ni wa jehanamu. Na zaidi hata ukiangalia wale wanafunzi wake ambao ndio mitume wa kwanza hawakuitwa Askofu, na zaidi neno Askofu au shemasi, hayana tofauti hawa ni watumishi watenda kazi ndani ya kanisa na ni watu wadogo, ni sawa na waimbaji, viongozi wa vijana, wa mama, wa baba au wapiga bendi na hawa wote wapo chini ya Nabii, Mtume, Mchungaji, Mwinjilisti na Mwalimu.
Sasa cha ajabu kazi alioifanya YESU na wanafunzi wake baada ya kuuwawa na watu wa dini nyakati hizo, wakaingiliwa na shetani na yeye akakopi hizo huduma tano akaongezea yake ya sita ambayo ni jina la wahudumu wa chini ndiyo akawapachika watu ya kuwa badala ya kanisa kiongozi wake awe ni Nabii na Mitume, akalipindua kwa jinsi hii na akalijenga kanisa lake akateua mwanadamu aitwe Askofu au Bishop ndio aongoze hizo huduma tano na hapa ndipo kanisa lilikosa mwelekeo sababu zile huduma tano ziliongozwa na askofu, na YESU hakuteua Askofu ndio aliangalie na kuliongoza kanisa. Natumaini unazidi kufunguka na kama YESU hajateua maaskofu katika huduma zake tano, sas jiulize hii huduma ya sita ndiyo mapenzi yake MUNGU? Najua hamjui ila amenituma niufichue uovu wa watu, mpone, hata wewe uliye na cheo cha Askofu nikuulize swali je Askofu ni moja ya huduma tano? Jibu hauna, kubali umetekwa na kama YESU hajaanzisha elewa sasa na wewe dhambi ya kuongeza neno la MUNGU imekushika kama ulikuwa haujui leo achana nacho ni machukizo mbele za MUNGU. Mpaka sasa unazidi kufunguka ufahamu wako.
Sasa nitakuelezea asili ya hichi cheo japo wengine mnalipenda ila laiti mngelijua usingekubali hilo jina ndio uitwe uwe kiongozi hii ni sababu ya kupokea mapokeo ambayo ni ya elimu ya wanadamu badala ya MUNGU. Sasa katika ufalme wa shetani yupo jini kubwa ambaye anaitwa NAPA, huyu ni jini ambaye yeye hutoa nguvu za kipepo kwa kila anayejiita Askofu au yeye ni Askofu ili awe kiongozi wa kanisa na ndio maana utashangaa maaskofu wanazo nguvu zaidi kuliko hao walioitwa kwa huduma tano, kazi yake huyu jini anapokaa ndani ya Askofu yeye anazivuruga hizo huduma tano na kuzidhoofisha na ndiyo sababu utaona watumishi wanaosema ukweli ni wachache na hata baada ya muda unakuta wamezimika na watu hushangaa ule moto aliokuwa nao uko wapi tena? Jibu unalipata hii ni sababu mtumishi anakubali kuwa chini ya Askofu huduma ya sita badala ya huduma tano au kwa lugha nyingine huduma ya Askofu awe ndio kiongozi wa kanisa hiyo huduma ya mpinga kristo na ni huduma ya 666.
Na pia katika ufalme wa shetani kuna jini anaitwa makeke, jini huyu yeye kazi yake kila aliye Askofu katika ulimwengu wa roho yeye ni mke wake huwaoa wanadamu hao katika ulimwengu wa roho na kimwili utaona maaskofu wamevaa pete hiyo ni maana yake uelewe. Na jini Makeke nilipokuwa nikiombana kupambana nae alisema siwaachi sababu wamesaini kuwa wao ni Askofu, na saini yenyewe na ile wanapo saini ili kukabidhiwa kanisa muda huo huo wanaichukua wanakaa nayo kama kiapo chako kati yako wewe na yeye. Hivyo mliokuwa hamuelewi sasa macho yafunguke na mpone sababu wapo waliopewa UASKOFU na wengine wanajiita wakiona ni cheo cha kumtukuza MUNGU kumbe ni cheo cha kumtukuza shetani, na YESU WA NAZARETI hana shirika na kiongozi ambaye siyo katika zile huduma tano. Nikuulize swali hauoni hapa hauna ujanja na umetekwa na wewe na umempuuzia YESU japo unalitaja jina lake, hata hiyo injili siku ile ya mwisho atakueleza sikujui sikujui, sababu moja wapo yeye hakuiamrisha hiyo huduma ili kulijenga kanisa sasa alichofanya shetani, akachukua jina la watenda kazi kanisani akalifanya ndiyo kiongozi mkubwa, je hiyo kazi itakuwa na YESU kweli? Wengi mmeshtuka ila mtukuzeni YESU ambaye ndiye mwalimu wangu, aliyenituma kwa mataifa yote niwaeleze habari njema za kweli na kuwatoa katika giza na mkatae kuongozwa na huduma tofauti na zile tano hata na zaidi shetani akabadilisha majina katika baadhi ya makanisa badala ya kuwaita Nabii, Mitume, Mchungaji, Mwinjilisti, Mwalimu, utashangaa mtu ni kiongozi wa kanisa anaitwa jina tofauti na biblia na zaidi hata kiongozi wao badala ya kuitwa Nabii au Mtume anaitwa jina tofauti, ukiona hivyo uelewe hayo ni mapando ya mpinga kristo, YESU hakuzileta hizo huduma zinazoitwa kwa majina tofauti.
Kama nilivyokwisha waeleza mara nyingi jinsi alivyoituma YESU soma makala yangu utafunguka na utubu leo. Mimi Hebron katika kanisa langu watu wanaoitwa shemasi au askofu kazi yao ni kusubiri maelezo kutoka kwa wachungaji, kufanya usafi, kukaribisha watu na kufanya kazi ndogo ndogo kwa jinsi mtu apendavyo. Hivi ndivyo inavyotakiwa ili YESU ainuliwe pamoja na kazi yake alioifanya yeye kuanzisha huduma tano. Na wanadamu muone aibu mbele za MUNGU kuongeza neno la MUNGU, madhara yake ni hukumu na hata hiyo kazi ya kuongeza huduma tano ni dhambi kubwa.
TUBU:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE HATA NIKAWA ASKOFU NA KUKUBALI, NAOMBA NISAMEHE, NILITEKWA NA SHETANI, NIKAPOKEA ELIMU YA MAPOKEO, NIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE, NAMKATAA SHETANI NA KAZI ZAKE ZOTE. AMEN.

NABII HEBRON.

[ad_2]