[ad_1]
Nawasalimu mataifa yote kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI ambaye ndiye aliyenituma kwenu wote mnaomtafuta yeye na hata msiopenda. Ila ninayo furaha kuu sababu amenituma habari njema na wote mtakaompokea na kumrejea yeye mtapona.
SOMA: WAGALATIA 1: 6-8, neno la MUNGU linasema:-
“Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.”
Hapo utaona biblia inaelezea tayari kuwa wapo watu wawataabishao wengine na watu hawa ni wale ambao wanahubiri injili ya namna nyingine ambayo imechanganya uongo na vipengele vingine. Uongo sasa injili ya jinsi hii kwa mhubiri anayehubiri huyo anaitwa mtaabishaji na tayari amelaaniwa na MUNGU. Injili kama zile ambazo watumishi wanahubiri makanisani halafu wanaabudu sanamu, kusujudu kina Maria, Mathayo, Petro na wengineo, hao wote wameshalaaniwa na hao waumini wanaoshiriki kuyapokea haya mafundisho ambaye yanaitwa habari mbaya yanawaua roho zao na wao wanashiriki hizo laana.
1 WATHESALONIKE 2:4
“Bali kama vile tulivyopata kibali kwa MUNGU tuwekewe amana injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao MUNGU anayetupima mioyo yetu.”
Na hapa utaona mitume nao wanasisitiza kusema injili ya MUNGU peke yake yaani mapenzi yake tu na siyo injili ya kuwafurahisha wanadamu wapendavyo. Mfano makanisa mengine hayataki habari ya wokovu, sasa ukishona hivi uelewe hao wameshalaaniwa na MUNGU sababu wameifuata elimu ya wanadamu badala ya kufuata neno la MUNGU peke yake. Embu chunguza ni maneno mangapi yapo hivyo na je ni mengi kiasi gani.
WARUMI 1:16
“Kwa maana siionei haya injili; kwa sababu ni uweza wa MUNGU uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.”
Neno hili lina maana kuwa injili ni habari njema kutoka kwa MUNGU na ni habari njema ikiwa tu neno lake litafuatwa kama lilivyo na lisichanganywe na uongo au mambo ya kuvunja amri za MUNGU. Injili inapokuwa tofauti haiitwi tena injili inaitwa habari mbaya, na inaitwa habari mbaya sababu MUNGU amekufuriwa au salitiwa na adhabu ya usaliti ukisoma katika kitabu cha Wagalatia 1: 7-8 utaona imeandikwa alaaniwe, watu wengi katika ulimwengu huu kwa sasa wamehubiriwa habari mbaya makanisani pasipo wao kujua. Amenituma niwaeleze habari njema ambayo ndiyo kweli yake yenye neno lililonyooka ambalo halina uongo wowote ni kweli tupu. Ili nyie ambao mlikuwa hamjui ya kuwa mmeiacha njia na kulaaniwa mumrejee yeye, na wale wanaofanya makusudi wakijua wanajenga ufalme wa shetani kwa kueneza injili ya uongo na kuwafanya mamilioni ya watu wapotee wasiingie mbinguni, OLE WAO. Ile siku ya mwisho watapambana naye msimamizi wa injili na sijui watamjibuje YESU.
Msifikiri YESU ni mpole, YESU ni mkali, ninamjua vizuri na hata anaponituma kwenu anaongea akiwa makini na yeye hakosei katika usemi wowote anaosema yeye palipo na ndiyo ni ndiyo, kama ni hapana ni hapana. Alipokwisha kusema na mimi katika habari hizi, akanifunulia niangalie injili inayohubiriwa katika nchi mbali mbali hata katika mikutano, akaniambia hiyo siyo injili yangu, ni habari mbaya na neno la MUNGU hakika halitarudi bure. Tazama hao wanaojilaani kila siku kila saa kuwataabisha mataifa, wanawapa elimu isiyo yangu na wanawapiga upofu kwa kuchanganya biblia baadhi sehemu chache na wamebadilisha. Akaniambia nikikueleza nimesalitiwa angalia sasa, na mimi ufahamu ukafunguka zaidi, akaniambia wanahubiri habari zangu halafu wanaabudu sanamu, wengine wanawachaji watu pesa ili wawaombee, wanawabariki watu wazima, wengine wanabariki pombe, wanafanya kanisa ni mahali pa biashara, wengine wanajiita majina ambayo siyo za huduma tano kama nilivyoacha, hao siwajui mimi, wengine wanafanya kazi hii sababu ya mshahara, wengine freemason, wachawi, wapinga kristo wengine ni wafisadi.
Hao wote wamelaaniwa na MUNGU tayari waeleze wasifikirie wanafanya kazi ya MUNGU, waeleze wazi wazi wala usipunguze lolote, wanamtumikia shetani na injili yao ni habari mbaya mbele za MUNGU.
NOTE:
Ndugu wasomaji wa makala ya Nabii Hebron, unapaswa umshukuru YESU kwa kunipatia habari njema ili ujielewe usije ukalaaniwa na wewe, na kama ulikuwa haujui sasa elewa na usishiriki ibada hizo kwa watumishi yeyote anayejiita kwa cheo chake, mchunguze, je analitendea neno kazi 100%, hasemi uongo na kuchanganya neno la MUNGU? Zaidi soma makala yangu utafunguka zaidi, yapo mengi sana aliyonieleza YESU, wewe soma ufunguke na uwatumie na wengine wasome ili wapone katika kudanganywa na hawa wanafiki na wauaji wa roho za wana wa MUNGU. Na je kutokana na haya yanayofanywa na wahubiri kwa njia ya uongo utabisha hawajalaaniwa? Na kama haujaokoka fuatilia sala hii:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU NAMKATAA SHETANI NA KAZI ZAKE ZOTE NA ELIMU YAKE YA UONGO, NIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE, UNILINDE, NIONDOLEE HII LAANA NA UNIONGOZE KWA ROHO WAKO MTAKATIFU ILI NIKAE SALAMA NA NIFIKE MBINGUNI SIKU MOJA. AMEN.
Karibuni mataifa yote katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE mje mponye roho zenu na mtengenezwe upya muwe sawa sawa na mumfuate YESU WA NAZARETI peke yake na niwaeleze habari zake. Ninamjua na nimemuona wala hafanani na zile picha za BRIAN DEACON aliyeigiza picha za sinema za YESU. Anawapenda, anasema mpeni mioyo yenu leo ili aishi ndani yenu.
NABII HEBRON.
[ad_2]