BILA KUOKOKA, NA UTAKATIFU, HAUINGII KWENYE LANGO LA MBINGUNI.

[ad_1]

Lango la mbinguni ndiye YESU mwenyewe ambaye atawaruhusu waingie wale tu ambao wamekubali kuifuata njia yake wakiwa hapa ulimwenguni, wameokoka na kuishi maisha matakatifu na walifuata njia yake yaani Neno lake bila kulibadilisha. Mfano lazima uwe umebatizwa kama yeye tena kwa maji mengi yanayotembea na siyo ya kisima. Watu wengi wanajiita wakristo wakidhani wapo salama yaani wakristo safi kumbe ni wakristo wachafu mbele za MUNGU, kivipi?
Alipokuwepo hapa ulimwenguni yeye mwenyewe KRISTO alisema tufuate njia zake, alimaanisha uyafuate aliyoagiza ndio utafika mahali alipo yeye, na yeye ndiye atakaye kufungulia mlango uingie mbinguni. Ila watu wengi wasipo mrejea YESU nawaeleza siku ya mwisho atawazuia kuingia mbinguni, na hata Neno linasema hivi; yeye ndiye atakaye toa hukumu na atatoa kwa haki, atamwangalia kila mtu je alifuata njia zake? Mfano yeye hakuruhusu ibada ya wafu sababu MUNGU siyo wa wafu bali ni MUNGU wa wenye hai, ila miungu ndiyo iliyo wafu.
Amua uokoke, ukristo bila wokovu ni sawa na gari bila kuwa na magurudumu au betri. Na wokovu safi haipo katika madhehebu wala dini bali ipo katika kanisa alilolijenga yeye, kama alivyolijenga ndani ya Petro. Cha kujiuliza madhehebu si yalikuwepo? Lakini kwa nini YESU akasema analijenga kanisa ambalo milango ya kuzimu hailiwezi? Ina maana madhehebu shetani anayaweza kuyaendeleza sababu siyo YESU kayajenga na zaidi MUNGU hana madhehebu, yeye analo kanisa tu.
Ila yapo makanisa ya shetani mengi sana na wakristo wanasali humo wakijua wanaenda kwenye lango la mbinguni kumbe ni lango la kuzimu. Hakuna kuokoka, pombe, ufisadi ni ruhusa. Sasa mfunguke, haya ni makampuni ya shetani ya kuuwa roho za wanadamu zaidi soma katika blog hii makala tofauti utapona roho yako. Wengi wameokoka wokovu feki, yaani wa jina tu hakuna matendo. Mtu wa namna hii hauingii katika lango la mbinguni ile siku ya mwisho
Amua uokoke, na YESU akae ndani yako na ufuate sheria zake, usidanganyike ukifa utaombewa, nakueleza muda ni sasa, ukifa basi. Kama una dhambi, jibu ni hukumu na kama hauna dhambi, ni mtakatifu utaenda paradiso. Mamilioni ya watu waliokufa tena wakristo maarufu na hata watumishi maarufu katika ulimwengu huu hawapo mbinguni, wapo kuzimu wanasubiri jehanamu. Sasa angalia na wewe utayekumbuka maneno haya, tena wanajuta, wanatamani watubu lakini haifai tena. Nimekupa siri hii uwaeleze na wengine, haya yote nilionyeshwa na YESU peke yake aliyeniteua nimtumikie, msidanganyike tena, tena wale walio watumishi katika ulimwengu huu 98% wanasubiri hukumu ule mwisho, mrejeeni YESU.
SALA YA TOBA:

BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE, UANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE, SIMTAKI SHETANI TENA NA VYEO VYAKE TENA. AMEN.

ZAIDI SOMA VITABU VYA NABII HEBRON MATOLEO YOTE UTAKUA KIROHO NA YESU ATAKULINDA HUKO HUKO ULIPO.

NABII HEBRON.

[ad_2]