UNABII KUHUSU ZANZIBAR TANZANIA VISIWANI 2014

[ad_1]

BY NABII HEBRON.
Kuhusu visiwa vya Zanzibar ambayo ni sehemu moja wapo ya nchi ya Tanzania. Kisiwa hiki ni tajiri sana ila utajiri wake ulikuwa umeibiwa na uthamani wake na pia maisha ya watu waliopo. Mwanzo wa tarehe 8.1.2014 MUNGU ameikomboa Zanzibar sasa ipo mikononi mwake na amerejesha uthamani wa Zanzibar na utajiri wake na maendeleo yake na ya watu wake. Mtaona mabadiliko makubwa sana kiuchumi, kielimu, na hata katika viwanja vya ndege. Mashirika mengi ya ndege kutoka nchi mbali mbali yatakuja na wageni wataongezeka zaidi. Uoto wa asili yaani mimea itastawi zaidi, na samaki soko litakuwa kubwa, wananchi watajituma sana kufanya kazi.
Katika serikali Mawaziri baadhi wataondolewa katika nafasi hizo, na pia katika bandari baadhi ya watumishi wataondolewa sababu kuna vitu vitafichuliwa. Uchawi haufanyi kazi tena katika kisiwa cha Zanzibar, waliozoea sasa mwisho umeshafika, ni MUNGU ndiye atakayeyafanya hayo yote na tayari ameshaanza kazi hiyo na atawatumia watu hao hao na kuwaongoza.
Madawa ya kulevya hayatapita tena katika airport na bandarini, MUNGU mwenyewe atafanya njia akiwa na YESU WA NAZARETI (Nabii Issa). Tanzania Bara nilishawaeleza yote yametokea na sasa ni wakati wa Zanzibar kuinuliwa juu, mtashangaa mabadiliko makubwa sana. Na pia mafuta ya petrol yapo ila yatapatikana pale wananchi wakijielewa maana wapo wanayo yamendea na waibe faida yote. Utajiri huu ni kwa ajili ya wananchi au watu aliowaumba MUNGU mahali hapo na siyo kwa wageni.
Mwaka 2015 viongozi wengi waliopo madarakani katika uchaguzi watalia machozi (hawatapata tena nafasi na watakaotumia uchawi) MUNGU atasimamia uchaguzi huu na atawaongoza watu aliyewaumba yeye wawachague wale watakao mtegemea yeye tu.
Zaidi soma katika blog ya Prophet Hebron www.prophethebron.blogspot.comna pia Prophet Hebron YouTube.
Uovu na ufisadi utafichuliwa kila mara katika maeneo yote na watasemana, myaonapo msiogope, mjue ndiye mwenyezi MUNGU yupo kazini. Hata pesa zilizoibiwa zikapelekwa nje ya nchi zitarejeshwa.
·        Bunge litakuwa kali sana, na MUNGU atawatumia watasema kweli bila kuogopa wala kusua sua.
·        Meli zitaongezeka.
·        Wananchi watajenga mahoteli makubwa yakitalii.
·        Biashara halali zitainuka na nchi nyingi zitaanza kwenda kufanya shopping Zanzibar kama ilivyo watu wanaenda Dubai au China. Hayo yote ni YESU WA NAZARETI ayafanya. Na Rais MUNGU atamuongoza wala hakuna atakayeweza kumyumbisha na atamlinda yeye peke yake.
·        Kuhusu kuvunjika muugano hilo halitakaa litokee milele ndivyo alivyonieleza MUNGU, na wanaotaka muungano uvunjike ni bora wakalime au kufanya biashara maana watapata faida. Ila kuhusu kuvunja muungano ni wanajisumbua akili zao, haya amenieleza yeye aliyeiumba Zanzibar na dunia yote, na Zanzibar ni sehemu moja ya Edeni ya sasa.
NOTE:
Ujumbe huu nimepewa mimi Nabii Hebron na MUNGU mwenyewe tarehe 8.1.2014, ndipo Zanzibar aliifungua upya na kuibariki na kuitoa mikononi mwa wakoloni walioiba uthamani wake na kwa watu wengine wenye nia mbaya. Zanzibar sasa siyo ile ya zamani ni mpya imeinuliwa juu na ipo mikononi mwake sasa.
MUNGU IBARIKI ZANZIBAR

NABII HEBRON WA KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.

[ad_2]