NABII HEBRON AAMBIWA NA YESU, BABA YAKE WA KWELI WA KIROHO NI MOSES KULOLA.

[ad_1]


Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron, Tokea YESU wa NAZARETI aniite kumtumikia muda mwingi kila mahali nilipokuwa ninasali  katika makanisa mbalimbali nilifikiri hao watumishi ndio walionizaa kiroho.

Na nilipokuwa katika huduma zao, nilikuwa nashangaa kwa nini wananiogopa hata kuniita majina ya muovu  na wakati sifanyi uovu , nilivumilia nilimuomba MUNGU  anichukue nirudi alikonitoa mbinguni maana napigwa kwa maneno mabaya na wachungaji, kwa kunisema vibaya mara nikiwa sipo ibadani  siku hiyo , ile siku nikija hata mchungaji au kiongozi wa kanisa hilo, hukaa na  mimi karibu sana kana kwamba ananipenda sana, ili nisiweze kuelewa au kuambiwa  na waumini jinsi alivyonisema.

Ila baadaye  waumini waliniambia kila kitu, nami nilimwachia YESU tu yeye ndiye aijuaye mioyo ya wanadamu, na ilifika  mahali hata mmoja  wa kiongozi  mkuu mwenye cheo cha Askofu katika kanisa la mwisho nililoabudu, kiongozi huyo nilimshangaa na yeye ananiogopa na angali nilikuwa mtoto mdogo kiroho tofauti na sasa.

Siku moja alikuja katika kanisa lake la mkoani kulikuwepo na ujenzi, akaniona nikamsalimia, kumbe moyo wake ulikuwepo na wivu kwa sababu aliona huduma yangu aliyonipa YESU, akamwambia mchungaji wake, hivi aisee kwa nini hadi leo hii hujamfukuza huyu Hebron?

Akamwambia huyu Hebron ni hatari hafai kuwepo katika kanisa langu, yule mchungaji hakukubali kunifukuza akaniambia “ achana naye wewe mwangalie YESU tuu.”

Nikaendelea kusali kama miezi minane hivi, na ilipofika September 2009, siku hiyo nilikuwa katika ibada ni siku ya Jumapili wakati wa kutoa sadaka akaja YESU mbele yangu bila mtu yeyote kumuona akaniambia  leo ndio mwisho wako kuja katika  kanisa hili, tena uondoke sasa hivi nitakuongoza cha kufanya.

Niliogopa  na kustuka sana, siku hiyo nilikuwepo na mmoja kati ya waumini anaitwa Charles nilikuwa nimeketi naye karibu, na yeye  baada ya kutoa sadaka  alitoka, alikuwa anaenda  moshi mjini na mimi  nilitoka nikaenda nae na ibada ilikuwa inaendelea.

Katika kuongea nakumbuka nilimwambia ila sikumueleza yote kwa undani, nikamwambia, nimesikia sauti imeniambia usirudi tena katika kanisa hili, wala usikanyage  hata mguu wako. Na ndivyo ilikuwa mwisho wangu na itakuwa milele kamailivyo na nilionywa na YESU WA NAZARETI.

Baada ya muda nikawa siendi kanisani nasali nyumbani na baadhi ya watu waliopenda kusali na mimi na kuwaombea, maana jambo hili la kuwaombea watu na kufunguliwa nilianza siku nyingi, na pale muumini alipokuwa akiombewa na mchungaji, akishindikana  akija nikimwombea anapata jibu hapo kwa hapo.

Nilichukiwa sana, nilifikiri ningetiwa moyo au waniinue huduma niliyonayo,  lakini walitaka kuniua kiroho ila kwa neema ya MUNGU, nilikuwa najua kabla ila hakuna neno kwa ujanja wakijua mimi sijui lolote kumbe najua kila kitu.

Ikafika muda nikawa nasema sasa YESU nitakaaje bila ya kuwa na Baba wa kiroho, akaniambia mimi ndiye Baba yako wa kiroho, achana na hao wewe mwenyewe ni shahidi kwa ajili ya hayo waliyokutendea, hao siyo Baba yako wa kweli wa kiroho, hawajui uchungu kuhusu wewe akaniambia, hao nilikupitisha tu huko ukaekae hadi wakati wangu ukifika nikutoe, hao ni Baba wa kambo wa kiroho.

Akaniambia, kama ilivyo kibinadamu mzazi wa kambo hawezi kupenda  kiukweli mtoto asiye mzaa yeye, akaniambia Hebron hivyo ndivyo ilivyokuwa. Basi nikapata amani nikasonga mbele na YESU akaendelea kunitunza na kunilea na kunifundisha kwa ajili ya kazi yake, mpaka ukafika wakati nikaacha kazi August 2011.  Nikabaki kuifanya kazi yake kama ilivyo sasa. Na ilipofika July 2012, akaniambia Hebron  sasa  nataka nikuonyeshe Baba yako wa kiroho aliyekuzaa wewe na ndipo ulipopokea huduma uliyonayo, nilishikwa na butwaa, akaniambia,

Huyu Baba yako wa kiroho amekuwa akiniomba sana kwa muda wa miaka  mitatu analia na kuomba kwangu kuhusu wewe, japo hajakuona kimwili ila anakujua hadi sura yako, ila  YESU akaniambia nilimwambia  subiri nianamtengeneza ikifika wakati wake nitakuletea na kukukabidhi, hapo bado hakuniambia ni nani?

Akaniambia Baba yako  aliyekuzaa wewe Hebron mtumishi wangu ni MOSES KULOLA, alikuzaa katika mkutano wa injili  N.M.C 1999, ndipo ulipopokea  huduma hiyo na mimi YESU nilikuwepo siku hiyo nikahakikisha umeipokea huduma ambayo MIMI na BABA  yangu MUNGU  tulipanga hivyo ila tulikuficha kama vile MUSA alivyo hifadhiwa kwa Farao na ilipo fika wakati akatoka huko, akaniambia na wewe ndivyo ilivyo, na wewe ni MUSA wa sasa.

Ikafika mwishoni mwa October 2012, akaniambia nenda ukamwone  Baba yako wa kiroho tayari sasa  anakusubiria kwa hamu na furaha, basi nikachukua hatua, nikamtafuta nikampata mtoto wake  anayeitwa kwa jina Willy, akanisaidia kufanya  mawasiliano na alipomwambia Baba yake ambaye kwa sasa ni marehemu yupo mbinguni amepumzika, akamwambia mwambie aje;  nikatii .

Alikuwepo Dar es Salaam nyumbani kwa Willy. Nikafika  nikaonana naye nikamwelezea alivyoniambia YESU, kuwa yeye ndiye Baba yangu wa kiroho, na mengine ambayo ni yangu na  MUNGU tuu, akaniambia  “umesema kweli” wewe ndiye niliomba muda mrefu , akaniambia ninakujua tena  mbele ya mtoto wake Willy,  basi akanibariki kama alivyoelekezwa na YESU na akaniambia uende RWANDA sikupata mtu wa kumtuma kwenda huko watoto wa MUNGU kule wanapotoshwa  hawajui tofauti ya shetani na MUNGU, wanaangamia.

Nikamwambia  pia YESU alishaniagiza baada ya Tanzania niende Rwanda. Siku hiyo ilikuwa tarehe 9.11.2012.  Na YESU akasema na yeye akamwambia mwanangu makao yako yapo tayari ila muda na siku ikifika mimi YESU nitakuja na BABA yangu kukuchukuwa, akamwambia tazama hata uliokuwepo nao katika injili wameniacha na umebakia wewe mwenyewe na akasema katika ulimwengu huu mumebakia watumishi wakubwa watatu tuu ambao hamjaniacha na katika Bara la Afrika  umebakia wewe peke yako tu, wengine wote wamenisaliti wamejiingiza kwenye freemason, wachawi, na kuirudia dunia japo wanalitumia jina langu, na mimi YESU nimekaa ole wao.

Akamwambia nimekuletea yule uliyeniomba kwa muda wa miaka mitatu na nikakuahidi, ndiyo Hebron mtoto wako, mbariki na umwongoze. YESU akaondoka, Mzee Moses akaniambia kwa mara ya pili tena piga magoti akanibariki tena na mke wangu na watumishi niliokwenda nao.

Toka siku hiyo ikawa ni furaha kwangu maana nililia kamasina Baba wa kiroho. Lakini haijalishi kwa sasa hatupo naye, ninacho waambia ukweli halisi msilie, mimi nililia nilipopata habari ya kifo chake, akaja YESU akaniambia usilie Baba yako yupo katika mkono wa kuume wa MUNGU, yeye ameshinda ulimwengu na yupo amestarehe anamtukuza MUNGU na kusifu, akaniambia kibinadamu inauma ila usiogope hii ni kwa sababu ulimpenda sana, akaniambia simamia kazi yangu na kusudi kama ulivyoelezwa na Baba yangu MUNGU na mimi YESU, akaniambia nilijua muda wake  umeisha hapa duniani  ndiyo maana nilikuagiza uende  na afanye kama nilivyomuelekeza kuhusu  wewe.

Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron mpaka sasa umepata picha kwa ufupi jinsi nilivyompata Baba yangu aliyenizaa kiroho.
Yeye alinipenda,aliniombea sana na kunifundisha mengi, na wala hakunionea wivu kwa ajili ya huduma aliyoiona ndani yangu ila alinikuza mpaka alipoondoka na sasa nimebaki na  YESU peke yake   tu, na MUNGU aliyeumba ulimwengu huu.

Najua kuna watu wengi wanampenda MUNGU ila wanagandamizwa na Baba zao wa kiroho, ukiona unagandamizwa ili usikue katika  huduma uliyonayo tambua huyo uliyenaye siyo aliyekuzaa kiroho, omba MUNGU, atakuonyesha baba yako.

Angalia mapito niliyoyapita  na ukiinuliwa na MUNGU  utashangaa wanaanza kusema ni mtoto wake wa kiroho. Usikubali hao ni wanafiki, songa mbele. Mbona kabla hujainuliwa walikukataa na kukulaani? Akili kichwani.

Malaika Gabriel aliniambia siku moja  MUNGU alisema na baadhi ya watumishi niliokuwa nikisali nao huko, ila mmoja akayahifadhi, waliambiwa jnsi huduma niliyopewa ni kwa ajili ya ulimwengu wote na hakuna atakayeimaliza kazi hii ni Hebron tu ndiye aliyechaguliwa, wao wakaingiwa na wivu, na wakakufanyia mabaya kwa ajili ya kusudi la MUNGU.

Neno la MUNGU lazima litimie tu na Hebronlazima itakuwa, MUNGU  hasemi uongo.

   
NABII HEBRON .

[ad_2]