MWANZO WA ANGUKO LA WAKRISTO KWA ULIMWENGU WOTE NI UBATIZO WA WATOTO WADOGO

[ad_1]

MWANZO WA ANGUKO LA WAKRISTO KWA ULIMWENGU WOTE NI UBATIZO WA WATOTO WADOGO


UFUNUO 13: 16,18
UFUNUO 19: 20

UFUNUO 13: 16, 18. Naye atawafanya wote wadogo kwa wakubwa na matajiri kwa maskini na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume au katika vipaji vya nyuso zao, hapa ndipo penye hekima, yeye aliye na akili na aihesabu ya mnyama huyo. Maana ni hesabu ya kibinadamu na hesabu yake ni mia sita sitini na sita.

UFUNUO 19: 20 Yule mnyama akakamatwa na yule Nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama nao walioisujudia sanamu yake, hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti.

Ndugu  msomaji wa blog hii ya Nabii Hebron,  mwanadamu uliyeumbwa na MUNGU kwa kila jinsi ya rangi zake tofauti apendavyo yeye. Ujumbe huu ni kwa ajili ya wanadamu wote, ujumbe huu nitakaoelezea jinsi wakristo walivyoangukia kwa idadi kubwa katika ulimwengu huu kwa kupigwa chapa ya Namba 666 bila kujua na kazi hiyo ikifanywa na watumishi wa uongo ( Nabii wa uongo) Ni mtumishi afundishaye mafundisho ya MUNGU asiyejulikana ikiwa ina maana hayapo katika Biblia, tofauti na Biblia ina maana yanatoka kwa MUNGU asiyejulikana yaani ( Baali).

Jinsi usomavyo wewe ujumbe huu , ndivyo na mimi Hebron nilivyoelezwa na YESU wa Nazareti uso kwa uso kwa hiyo kazi kwako usije ukalia siku ile ya mwisho au endapo utakufa kabla ya kutengeneza na yeye muda huu .

Anguko kwa wafuasi wanaompenda YESU lilianza kwa jinsi hii, kwa kuanza kubatiza watoto wadogo , badala ya mtu mzima na akili zake akubali mwenyewe abatizwe kwa maji mengi tena mtoni kijito cha utakaso wala siyo kisimani.

Nitaelezea kwa ufupi lakini utapata picha. Mtoto mdogo anatoka kwa MUNGU, ndipo anakuja ulimwenguni na akizaliwa na anapokuja ulimwenguni anakuwa anao malaika kutoka kwa MUNGU ambao humlinda na kuhakikisha yale yote yaliyo kusudiwa na MUNGU  kwa kiumbe hicho yani mtoto yanatimia katika ulimwengu huu na ule mwisho wake mtoto huyo anarudi kule alipotokea yani mbinguni.

Mfano halisi ni YESU WA NAZARETI alitoka mbinguni na akarudi mbinguni na hata Herode alipotaka kumuua wale malaika waliokuwa na YESU walimlinda na kuwaongoza wazazi wake,  pia   hata mama jusi walionywa wasirudishe ripoti kwa Herode.
Huu ni mfano tu nimekupatia uzidi kuelewa na ufunguke ufahamu wako, hakika utaona jinsi watu walivyopotea na wanavyoendelea kupotea na kazi hii ya kuwaharibu  wanadamu inafanywa na Nabii wa uongo ( mtumishi au watumishi wanaofundisha tofauti na Biblia na kuibadili na kukushirikisha mapokeo yasiyojulikana yalipotokea hayo ndiyo ya MUNGU asiyejulikana yaani ( Baali).

Nitaelezea kinachofanyika kwa mtoto mdogo anapopelekwa kanisani na kumwagiwa yale maji, kinachofanyika kupitia yale maji na anayefanya hayo ni mtumishi wa uongo kwa sababu Biblia haijaruhusu mtoto mdogo abatizwe.

Tafuta kwanza kitabu cha mwanzo mpaka mwisho. Jibu hakuna,  tunatakiwa tumfuate YESU yeye ambaye ndiye njia ya uzima na kweli kiimani na kimatendo, na hakuna pa kumlaumu YESU yeye alionyesha njia na mfano akasema afuatwe yeye ndio kweli katika mambo yote sasa imebadilika, imekuwa kinyume ila imeandikwa Neno lake lazima litimie na halitarudi bure na imetimia kwa kupigwa chapa  usoni  ya namba 666. Hii namba  666 ni roho, usifikiri utaandikwa usoni kimwili, maana hakuna apendaye aangamie ila mambo haya hutendeka kwa roho, na hii roho ni ya shetani, ambayo huwekewa mtoto mdogo akiwa anabatizwa    kama tunavyo au tulivyokuta katika makanisa unaitwa ubatizo na kumbe siyo ubatizo, maana ya ubatizo ni kuzamishwa, hii yenyewe kibinadamu pamoja na akili yako ukiangalia maana yake utajua  ni uongo mtupu. Ila imebadilishwa kwa kufungwa fahamu za wanadamu ikaitwa ubatizo badala ya chapa 666 ya mpinga Kristo.

Ukisoma katika Ufunuo 13:16, 18 na Ufunuo 19: 20. Utaelewa vizuri. Sasa kinachofanyika mtoto mdogo akimwagiwa yale maji ndani yake yanakuwa na hiyo roho ya shetani kwa sababu siyo mpango wa MUNGU anayejulikana watoto wadogo wabatizwe, ila watoto wadogo inatakiwa wawekwe wakfu tu yani kubarikiwa kama ilivyofanyika kwa YESU WA NAZARETI  akiwa na siku nane. Mtoto huyo anapobatizwa hayo  maji kama nilivyokwisha kukueleza pale tu anapowekewa kichwani, wale malaika kutoka kwa MUNGU waliokabidhiwa mtoto huyo,huondoka na kumwacha, maana yale maji yanakuwa  na roho ya shetani na mtoto huyo huwekwa alama ya namba 666 bila ya watu kujua, na afanyaye hayo  imeandikwa katika ufunuo 19 :20  ya kuwa ni Nabii wa uongo ndiye atakayefanya hayo akishirikiana na mnyama ambaye ndie shetani, na haya hufanyika katika roho siyo mwili ndio maana Neno la MUNGU linasema vita vyetu siyo katika mwili bali ni katika roho na ndivyo pia imeandikwa usiziamini kila roho bali zichunguzeni kama kweli zatoka kwangu, roho kutoka kwa MUNGU haziwezi kumpinga MUNGU ila ambazo zimetokea kwa Mungu asiyejulikana hizo ndizo za shetani, mfano kuabudu sanamu, ubatizo wa watoto wadogo.

Ndugu msomaji haya ninayokuelezea mimi Hebron siyo maneno yangu ni maneno aliyonieleza YESU na mimi nakufundisha ili watu wapone wasiangamie ila ni kwa wale tu watakao tii ila watakao kaza shingo zao kuwa ngumu hukumu ipo tayari juu yako, na wote wanaobatiza watoto wadogo ubatizo tena ambao haupo katika Biblia yaani MUNGU anayejulikana na kuleta ubatizo ambao haupo katika Biblia yaani haujulikani ulipotokea, ( Ndiyo MUNGU asiyejulikana) na wewe ukafanyika uunganishwe kwa Mungu asiyejulikana na ile siku ya mwisho utapelekwa huko huko pasipo julikana.

Wote tunajua mtoto mdogo anaitwa malaika wa MUNGU, hii ni sababu hajui kutenda dhambi na anakuwa yupo na malaika kutoka kwa MUNGU na ndiyo maana humlinda, na zaidi mtoto mdogo hata mchawi  akiwanga ndani ya nyumba huanza kulia ila watu hawaelewi, anaona adui, hii yote ni sababu bado malaika wa kumlinda wapo na yeye  ila mara anapowekewa yale maji tu kanisani malaika humuacha, maana anakuwa siyo mali ya MUNGU tena amekabidhiwa shetani, na jinsi hii ilifichika sana na watu hawakujua ila YESU amenifunulia siri hii na zaidi soma kitabu changu cha UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE.  Utaelewa zaidi.

MARKO 10: 42

NOTE:

  1. Kuanzia sasa utambue unapompeleka mtoto mdogo abatizwe kwa maji yale ujue mtoto wako anaenda kuwafukuza malaika aliotoka nao kwa MUNGU, na shetani kummiliki na kumpiga chapa 666.
  2. Usidanganyike eti akifa  akiwa mdogo hataenda mbinguni, kabla hajabatizwa huo ubatizo wa maji ya kichwani. Jambo la kwanza atakuwa bado yupo na wale malaika aliotoka nao mbinguni watamrudisha alipotokea na hatapotea. Ila ubatizo huo wa Mungu asiyejulikana na wewe ukifa utaenda huko kwa Mungu asiyejulikana.  Amua leo umtake  uende  kwa Mungu anayejulikana? Au asiyejulikana uamuzi unao mwenyewe ndani ya moyo wako, maana kila mtu atasimama peke yake kujitetea siku ile ya mwisho.

  1. Madhara yake kuwabatiza watoto wadogo ndiyo maana wakristo wanakuwa  
      waovu hata hawafananishwi na jina la Kristo ambaye ni Mtakatifu, inabakia jina  
      tu bila uthamani wa nguvu za YESU ndani ya mkristo.Na pia hofu ya MUNGU
      inakuwa haipo ndani yao na matendo maovu huwa ni jambo la kawaida kwao.

Sasa ninayokueleza uelewe wala mimi siogopi kusema kweli na hakuna atakaye jaribu kunizuia kusema kweli ya YESU wa Nazareti na kama yupo ajaribu, atakutana na MUNGU mwenyewe asifikiri anapigana na Hebron ni MUNGU hakuna atakaye weza kumpinga wala yeye  hashindwi na lolote ni MUNGU mwenye uwezo wote, yeye ndiye aliyeagiza watoto wadogo wabarikiwe tu! Sasa kwa nini watumishi wa uongo wanawabatiza watoto wadogo? Wanatumika kuwapiga watu namba 666.Tambua mtu yeyote katika ulimwengu huu aliyebatizwa ubatizo wa kichwani huyo tayari anayo alama ya namba 666 na tayari hao wanadamu wamepewa shetani bila ya wanadamu hao kujua. Sasa mfunguke watu wote wa ulimwengu wote YESU wa Nazareti ameniambia msikubali tena huo uchafu hilo ni kaburi au jehanamu,  ile siku akija YESU atawaangalia wote wenye alama yake tu ndio atakao wachukua je nikuulize swali? Sasa kama unayo alama ya 666 atakuchukua? Jibu hapana.

  1. ONYO:
       1. Ole wao wawawekeao wanadamu  aliowaumba   MUNGU namba 666. hukumu 
            ipo tayari juu yao,


          
       2. Hao wanaobatiza ubatizo watoto wadogo ubatizo huo YESU kawaambia 
           haujatokea kwa BABA yake ambaye ndiye MUNGU anayejulikana. Ila umetoka
           kwa MUNGU asiyejulikana wala kujibu ( Mungu Baali) na wote mnaoshiriki 
           ibada hizo hamwongozwi na MUNGU aliye hai, mnaongozwa na Mungu asiyejibu 
           na asiye julikana yaani ( Baali) na  nyie kufanyika watoto wa Baali bila kujua,
           badala ya kufanyika wana wa MUNGU anayejulikana.

  1. Shetani aliifunga hii siri  98% katika ulimwengu wote na makanisa yakawa siyo 
      makanisa tena ni pango la unyang’anyi (Baali ndiye kiongozi ). Sasa YESU 
      amenituma niufichue uovu wote ili watu wapone, maana baadhi ya watumishi
      aliniambia  aliwatuma wakakataa kusema na yeye amewakataa tayari. Ila

NOTE: Usikubali kubatizwa ubatizo usiotoka kwa MUNGU anaye julikana, hata hao wanaobatiza ubatizo huo hawajulikani na YESU na siyo wanafunzi wake 100 %. Wangekuwa wanafunzi wake wa kweli wangefanya kile alichofundisha mwalimu YESU wa Nazareti. Sasa wanafundisha yale ambayo siyo yake na kamasiyo yake yaani yeye njia ya uzima  na kweli utafika alipo yeye? Jibu hapana.

Imeandikwa watu hawa huniabudu kwa midomo tu ila ndani yaoni mbwa mwitu na mimi sipo nao. Tokeni huko mkatengane nao hao ni mbwa mwitu watumiwao na shetani katika kanisa ili kuziua roho za watoto wa MUNGU. Ndiko huko kuwapiga chapa hasa katika mwisho wa mwaka ndipo hufunga hesabu yao na kumpatia shetani ya kuwa mwaka huu hawa ndio wamewapiga chapa ya namba 666 ni wake. Usikubali ewe mwanadamu huo ndio ukweli na haitabadilika. Neno lake lazimalitimie na haya niliyokueleza ni ya MUNGU anayejulikana.


NABII HEBRON

[ad_2]