[ad_1]
NABII HEBRON AKIWA NA BABA YAKE WA KIROHO ALIYEMZAA- MOSES KULOLA.
Ndugu msomaji wa makala hii, habari hizi ni za kweli. Mnamo tarehe 3.8.2013, BWANA YESU alipokuwa akinifundisha kuhusu kazi yake na jinsi ilivyoharibika, watumishi wameshabadili neno lake na kuwa kinyume na yeye alivyopanga yeye ambaye ndiye njia ya uzima na y a kweli, wengi wamekuwa wachawi na kujiingiza kwenye chama cha freemason cha shetani. Ila shoka lake tayari lipo juu yao, maneno haya nimemnukuu, kama alivyonieleza ukiamini sawa ukikataa shauri lako, utakuja kulia kama hao viongozi . (Marais na wafalme wa n chi mbalimbali katika ulimwengu huu wanateseka sana kuzimu), wakiwamo wanajimu wote katika dunia hii, wote waliokufa wamekataliwa na MUNGU wanateseka mateso yasiyoelezeka maana niliwaona kwa macho yangu japo na viongozi wa dini wengi 99 % waliokufa wamekataliwa na baadhi ya wanamiziki maarufu duniani waliokufaga wote wapo kuzimu, wanateseka mateso yasiyoelezeka wanatamani hata kuja huku duniani wa waonye msitende dhambi na kila miziki yao ikipigwa huku duniani ndivyo wanavyoteseka zaidi.
Ila mlango nulishafungwa na malaika Mikaeli hakuna kutoka. YESU akaniambia nimekuonyesha ili uone hali halisi jinsi watu wanavyoangamia kwa dhambi, wameacha kutengeneza maisha yao wanajidanganya wakifa watafanyiwa ibada za wakfu na maombezi , YESU wa Nazareti akaniambia anayenitaka sasa hivi ndiye ninaye mtaka mimi. ( Akaniambia anitafutaye kwa bidii ataniona ) na anayesema muda bado atanitafuta baadaye na mimi huyo simtaki.
Akaniambia ndivyo ilivyo kwa hao marais wa nchi mbalimbali nimekuonyesha uone hali halisi. Akaniambia hawa maraisi walio nikataa mimi walikuwa wamejieleza kuwa wakifa wataombewa na watapokelewa , na ni makanisa kupitia watumishi watumishi wasio sema kweli na kuwapoteza watu wasitengeneze maisha yao kwa kunirudia mimi kwa kunirudia mimi YESU, akaniambia soma katika kitabu cha Waebrania 9:27-29 Imeandikwa hivi , kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja , na baada ya kufa hukumu, kadhalika KRISTO naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi atatokea mara ya pili, pasipo dhambi kwa hao watazamiwao kwa wokovu (Hapa utaona Neno linasema ukishakata roho tuu, kama hujatengeneza na y eye kinachofuata ni hukumu).
Sasa ndugu msomaji wa nchi yeyote , taifa lolote na bara lolote, kilicho waponza hawa viongozi au watu maarufu kukataliwa na MUNGU walivyokuwa hai walitegemea ibada za wakfu, na ibada za mazishi yao wataombewa na watumishi wengi na watu wengi hivyo watapokelewa. Kwa MUNGU siyo hivyo, hizo ibada za wakfu ni ujanja wa shetani kuwapumbaza watu ili wasiurithi ufalme wa MUNGU. Niliogopa sana akanionyesha, embu angalia mazishi na ibada kubwa zisizo elezeka za kufana wakati marais hawa na wafalme wakizikwa. Je ! kwa nini hawajapokelewa paradise,? Si kuwa na jibu, akaniambia muda wa watu kunifuata mimi YESU na kunipata ni sasa, hawa wengine wanategemea wataombewa na watu wengi na nyimbo zitaimbwa na makaburi ya kifahari na wengine hata wanakaushwa ili wasioze, lakini MUNGU haangalii hayo.
Akaniambia waeleze watu wote habari hii hata wasiokujua wote ni watu wa MUNGU anayetaka kupona apone atakaye kaza shingo yake kuwa ngumu shauri yake, ( KUZIMU NA JEHANAMU INAWASUBIRI). Ni mekuonyesha hayo ili ujue namna ya kuueleza ulimwengu wote na ole wake atakayejaribu kukuzuia, kwanza hataweza na pili itakuwa ndiyo mwisho wake kuishi katika ulimwengu huu ni yeye YESU ndiye atakaye mshughulikia haijalishi upo mwenyewe kimwili.
Mwanadamu ni nani hata ashindane na mimi MUNGU? Mimi ndiye niliyemuumba na nikitaka muda wowote naweza kumuangamiza. Akaniambia Eliya kipindi kile alikuwa mwenyewe kimwili na mabaali walikuwa 450, ila Eliya aliwaangamiza. Akaniambia naelewa na ninaona kila kitu hapa duniani. Na ndivyo itakavyokuwa songa mbele waeleze watu ukweli usiogope mtu yeyote, shetani amewateka watu wengi sana na hawajijui. Tazama ni miaka 64 imepita toka mwaka 1949 hakuna Rais aliyeenda paradise wanasubiri hukumu siku ya mwisho.
Enyi wanadamu tengenezeni maisha yenu msije mkaangamia mkidhani mkifa mtafanyiwa ibada mtakubaliwa, nakupa mfano je wewe, uliye mtu wa kawaida hutaki kutengeneza maisha yako je wewe utaombewa na watu wengi kama inavyofanyikaga kwa marais au wafalme? Jibu hapana, wao waliombewa na watu wengi na siyo ajabu maombi ya nchi nzima ila wamekataliwa! Je wewe unayeombewa na watu wachache utapokelewa? Jibu hakuna.
Alipomaliza kusema na mimi akaniaga akaniambia mwanangu, mimi ninarudi kwenye kiti cha enzi nitakuja tena wakati mwingine. Niliduwaa nikarudisha picha za mazishi ya viongozi wa nchi mbalimbali pamoja na maombezi yote, hakuna kitu na jumla ya miaka 64 imepita katika ulimwengu huu hakuna RAIS au mfalme aliyepokelewa na MUNGU hata wale walionyongwa au kuuwawa. Kweli MUNGU ni wa haki upandacho ndicho utakacho vuna, ukipanda dhambi utavuna hukumu, ukipanda mema paradiso.
Nawasihi wanadamu wote huu ni wakati okokeni tengenezeni maisha yenu ukisha kata roho tu basi, haki yako inakusubiri kama ni hukumu au paradise. Msidanganyike eti mazishi yalifana na maombezi. MUNGU anaangalia yule aliyekufa. Kila mtu atasimama mbele za YESU kusomewa mashitaka yake na hakuna wa kukutetea hivyo ndivyo fomula ya MUNGU.
Hesabu hizi za kipindi cha miaka 64 tokea mwaka 1949 hadi tarehe 3.8.2013 hakuna Rais yeyote aliyefariki aliyepokelewa paradise.na ni wengi sana . MUNGU haangalii cheo, utajiri wako ni uhusiano kati yake na wewe tu.
Mwisho wa nukuu , Nukuu ya YESU wa Nazareti.
NOTE:
Miaka hii yote 64 ni ulimwengu wote , ukitaka kujua Rais aliyekufa au mfalme chunguza kama alikufa kati ya kipindi hiki 1949- 3.8.2013. utaujua ukweli.
Mrudieni YESU watu wote wa ulimwengu, kuitwa mkristo tu jina siyo tiketi yako ya kwenda mbinguni. Ni Wokovu na Utakatifu tu.
NABII HEBRON.
[ad_2]