NDOA ZINAZOFUNGWA NA MAKANISA YA SASA NI NDOA ZA MATATIZO NA SHIDA

[ad_1]

Ndoa ni huduma kamili aliyoianzisha MUNGU mwenyewe, na kwa nia njema kwa ajili ya utukufu wake na siyo utukufu wa chochote kile, na yeye ndiye msimamizi wa ndoa na mshauri wa wanandoa, ambao ni kati ya mwanaume na mwanamke kuungana na kuwa mwili mmoja. Ila kwa sasa imekuwa kinyume na nia njema aliyoipanga kama baraka za ndoa ambazo ni amani, furaha, uzao mwema na mafanikio ya kiroho na ya kimwili.
Jambo la kwanza, kanisa la sasa badala ya kufungisha kwa agano la baraka kama inavyoonyesha katika kitabu kitakatifu, mtumishi anakupa kiapo cha shida na raha, ile tu mwanandoa anapokiri agano la shida tu, tayari shetani anashikilia ya kwamba shida imeruhusiwa katika ndoa hiyo na matokeo yake  ndoa zinakuwa ni shida tu, na huu ni mchomeko wa shetani aliouingizia  katika ya ndoa, muumini akishafungiwa ndoa kwa agano la shida, hapo hakuna ujanja lazima hiyo shida ikufuate na sio mpango wa MUNGU ndoa watu wafungiwe kwa agano la shida. Tafuta katika BIBLIA  kitabu chote ndoa zote zilibarikiwa tu, na hawakuambiwa wakawe na shida, sasa hizi shida wala hazijaandikwa katika kitabu cha BIBLIA (au tuite ndicho kiongozo cha maisha ya mwanadamu alivyopanga MUNGU) sasa mnaona hapa kanisa limetekwa na shetani na kuruhusu ndoa ifungwe kwa agano la shida. Inabidi agano hilo livunjwe kinyume na hapo shida haitoondoka milele, maana umeikiri wewe mwenyewe na ukasaini na shetani ameshikilia bango, ndoa kuwa na matatizo kiasi kikubwa kimesababishwa na wanaowafungia ndoa wanawalaani wana wa MUNGU, na ndiyo maana watu au wachumba unakuta kabla ya kufunga harusi, unakuta wanao upendo na mafanikio ila wakishafunga ndoa tu  maisha yanaharibika na kubakia watu kujilaumu na majuto, na kanisa lilivyopigwa upofu halishtuki limekosea wapi. Mwana ndoa na wewe unayetarajia kufunga ndoa usikubali kufungiwa ndoa kwa agano la shida kama unaipenda ndoa yako. ( Mwanzo 24: 60) wakambarikia Rebeka wakamwambia, ndugu yetu, uwe wewe mama wa kumi elfu mara elfu nyingi na wazao wako waurithi mlango wa hao wakuchukiao. Hapa tunaona Rebeka alivyoolewa alibarikiwa na kutamkiwa mema, na baraka. Je huyu YESU ndiye anaruhusu ndoa zifungwe kwa shida? Jibu siyo yeye na ndoa za namna hiyo zinazofungwa kwa agano lashida. MUNGU hashiriki na ndiyo maana mabalaa na mikosi ambazo ndizo baraka za shetani hutawala, ila ole wao wanaoiharibu huduma hii aliyoianzisha MUNGU kwa kuongezea maneno ambayo siyo MUNGU ameruhusu watoto wake walaaniwe (Ufunuo 22:18-20).
Mfano mwingine ni katika kitabu cha Ruthu( 4:11-12) hapa pia soma katika BIBLIA yako utaona ni baraka za ndoa tu na siyo shida.
Zaburi ya( 127:3) MUNGU anaelezea uzao wa tumbo ni thawabu yani baraka ila badala ya watoto kuzaliwa na baraka nao pia wemekuwa wamekirishwa hilo agano la shida katika uzao wao, ndio maana watoto pia wanazaliwa na kuwa kero au shida, wanatabia mbaya, wezi, wavutaji bangi, na tabia nyingi tu chafu. Hii ni kwa sababu ya agano la shida, unabakia kuchapa na kupiga watoto na hata kujuta kwa nini amewazaa, hii yote ni majibu ya kufungishwa ndoa kwa agano la shida na zaidi agano hili linarithi unafuata huo uzao wote. Zaburi ya ( 128.3) mkeo atakuwa kama mzabibu wa nyumba yako, wanao kama miche ya mizaituni wakiizunguka meza yako. Ina maana mke ni baraka kwa mume pamoja na watoto. Ila asilimia kubwa siyo baraka ni shida tuu mpaka vyakula mezani havipatikani ni upungufu tuu. Hii yote ni sababu ya agano la shida, na YESU anachukizwa sana na jambo hili, ameniambia niwaambie kweli mpate kupona na mimi nawafunulia haya kama alivyoniambia wala sipunguzi wala kuongeza. Ndoa za agano la shida hizo sio ndoa za MUNGU alizozianzisha, hizo ni ndoa za akili za wanadamu kupitia shetani. YESU aliniambia maneno haya kwa uchungu mkubwa sana ikiwa inamaanisha watoto wake wanafungiwa shida nao hawajijui. Jambo lingine YESU akaniambia nafasi yake katika ndoa amepewa mwanadamu badala ya YESU yani “bestman” mwanaume na mwanamke. Hawa huitwa wasimamizi wa ndoa, hii ni makosa na machukizo  na siyo mpango wa MUNGU, YESU peke yake ndiye mshauri salama na hawezi kukusaliti ila mwanadamu atakusaliti tu. Na yeye hana baraka hizo za YESU, na zaidi utamkuta huyo “bestman” hawawapendi kutoka rohoni, au wanawaonea wivu hao wana ndoa, au unakuta hao wasimamizi wanawaloga au hata kuwasengenya hao maharusi, na wasimamizi wengine ni wakununuliwa kwa pesa na wengine husimamia tu kwa sababu ya kupata kitu fulani mfano suti, viatu na jambo lingine wanandoa hao wanapokuwa na matatizo na kuwashirikisha wawasaidie unakuta ndio wanaoibomoa kabisa. Natumaini unazidi kuelewa kuwa ni YESU tu  ndiye mshauri mwema wa ndoa.
Jambo lingine YESU anachukizwa sana na watu kufunga ndoa na mimba na watumishi wanahalalisha. YESU hahusiki na uzinzi, hiyo mimba ni matunda ya uzinzi ambayo imevunjwa amri ya MUNGU halafu inakuja kuhalalishwa kanisani, ndoa hizo ni feki na hata kwenye mafaili ya MUNGU mbinguni na laana na huyo anayeipitisha na yeye anashiriki laana hiyo na hiyo sio ndoa takatifu ni ndoa chafu mbele za MUNGU. MUNGU haruhusu uzinzi, leo hii kanisa linaruhusu watu kufunga ndoa na mimba! Huu ni utaahira kabisa na kumdharau MUNGU na sheria zake.Watu wote dunia nzima waliofunga ndoa takatifu ya MUNGU, Hizo ni ndoa za akili  za wanadamu na MUNGU hazitambui hata hao wanaozifungisha haijalishi wanalitaja jina lake MUNGU hawatambui.
Nikuulize swali MUNGU anaruhusu uzinzi? Na je kazi ya kanisa ni kuhalalisha uzinzi? Na kanisa hilo ama watumishi wanaofungisha ndoa hizo za uzinzi hao ni watumishi wa  MUNGU mtakatifu au mungu mchafu? Jibu ni mungu mchafu ambaye ndiye shetani na pia mpinga KRISTO, hii yote kwenda kinyume ni kumpinga KRISTO, na hao wafanyao hayo hao ni wapinga KRISTO, haijalishi wanalitaja jina la YESU, je hayo ndiyo matunda ya YESU? Jibu siyo. Na wewe ujue ndoa hizo ni za matunda ya shetani, ndoa za agano la shida, kufunga na mimba.
Ndoa za mashoga, ndoa za wanandoa kulogana na kufanikiwa kuoana hizo ni za shetani. Na hazitakuwa na baraka daima. Na zaidi MUNGU amesema ndoa iheshimiwe na watu wote, hii ina maana hata watumishi waheshimu taratibu za MUNGU ila wameacha kuiheshimu huduma ya ndoa kama MUNGU alivyopanga na kuudharau, na badala yake kuwafungia agano la shida, hii tayari ndoa haijaheshimiwa sawasawa na kusudi la MUNGU alivyotamka.
Sasa kama unamdharau MUNGU, je wewe ni mwanadamu wa aina gani? Kama ulikuwa haujui sasa umejua, acha. Na kama unaendelea, hukumu inakusubiri. Watoto wa MUNGU hawakuumbwa kuja kulaaniwa madhabahuni kwa agano la shida  yeyote.  Injili imebadilishwa tofauti na MUNGU alivyopanga na kama imebadilishwa kinyume na yeye na akaonya ole wake atakayeongeza au kupunguza maneno ya kitabu hiki, shimo la moto linamsubiri, na wengine wafanyao kazi yake kiulegevu hao atawalaani mwenyewe, kiulegevu ina maana nyingi. Kuupinga mpango wa MUNGU na siku ya mwisho atakuambia sikujui sikujui mimi.

[ad_2]