ALIYONIELEZA PETRO MWANAFUNZI WA YESU WA NAZARETI

[ad_1]


BWANA YESU asifiwe! Kama nilivyokwisha kueleza mara nyingi jinsi YESU alivyoniita na kuonana naye uso kwa uso na kunituma kuifanya kazi yake kama anavyotaka yeye ili aukomboe ulimwengu na kuupindua ufalme wa shetani, pia alinikabidhi kwa serikali yake ya mbinguni, ninawajua kwa macho ya nyama na ndiyo ninaofanya kazi nao. Nitaelezea kwa ufupi tu kwani hayo mengine ni yangu peke yake.
                                                                                           
Mwanafunzi huyu ambaye ndiyo Simon Petro ukisoma katika nyaraka utaona ndiye mwanafunzi ambaye YESU alilijenga kanisa ndani yake ambalo milango ya kuzimu haitaliweza milele. Ni jasiri ajabu, nakueleza upate picha halisi. Nitakuelezea point moja tu katika yale aliyonieleza wakati akinifundisha jinsi ya kuifanya kazi ya MUNGU.
Akaniambia Hebron usiogope natamani nishuke nije ulimwenguni tuifanye kazi ya BABA ila usiogope haiwezekani nitakuja ule mwisho. Akaniambia leo hii wewe ndiye Petro wa sasa ujijue hivyo, ndani yako limejengwa kanisa ambalo ni MWAMBA na ni MUNGU peke yake ndiye kalijenga. Muda wangu nilipokuwepo hapa ulimwenguni niliitetea injili, hata soma katika nyaraka utaelewa na kuona japo hayo ni machache tu yaliyoandikwa. Na wewe utafanya zaidi maana utukufu wa kanisa la mwisho ni mkubwa kuliko wa kwanza sababu ni kwa ajili ya maandalizi ya ujio wa YESU na mwisho wa dunia. Akaniambia, wapo watakao mpinga YESU na wapo watakao mkubali YESU, hata kipindi changu ilikuwepo hivyo hivyo ila wale walio wa MUNGU watapona wale watakao kusikiliza na kumrejea MUNGU aliye hai, maana kwa sasa tupo mbinguni tukiangalia mambo yanayofanyika makanisani ni machukizo tupu 98% all over the world ni elimu ya binadamu inawaongoza ambayo siyo elimu ya MUNGU na watu wamepigwa upofu biblia imebadilishwa.
Akanaimbia makanisa yote yasiyoenenda sawa na Neno la MUNGU makanisa hayo yamekuwa ndiyo malango ya kuzimu na makanisa hayo yanaoperetiwa na mpinga kristo maana makao ya mpinga kristo yapo kuzimu, na watu wakiyasikiliza na kuyafuatia hayo mafundisho tayari na wao waumini wamekuwa wapinga kristo au adui wa YESU, japo wengi hawaelewi na mimi nakueleza uelewe na uwafundishe watu wapone roho zao maana hawapo katika kanisa lenye malango ya  mbinguni ila wapo katika makanisa ya malango ya kuzimu yaani njia ya jehanamu.
Akaniambia mimi enzi zangu nilipambana nao na sikukubaliana nao kwa ajili ya uongo (mafundisho) na kwenda kinyume , na japo iliandikwa kifo changu nitauwawa na kuwekwa msalaba kichwa chini hiyo ilitamkwa na ikatimia na sababu zilizonifanya niuwawe na Waroma ni sababu nilikataza watu wasiabudu sanamu wala miungu na YESU siyo sanamu. Sasa sababu mimi naujua ukweli na YESU WA NAZARETI alinifundisha na nikaujua ukweli na watu wakabadilika, sasa Waroma na miungu yao na shetani, mambo yao na kazi zao ziliharibika na ndipo wakaniua mimi ambaye ndani yangu YESU alilijenga kanisa, na kile kitendo cha kuniua mimi ilikuwa inayo maana ya kuuwa ukristo hapa duniani na zaidi hata mahali walipozika mwili wangu ilikuwa inayo maana kubwa katika ulimwengu wa roho yaani yale aliyoyaweka YESU japo Petro amekufa umebakia mwili, labda ilo kanisa litakuwepo katika hiyo maiti.
Wakanizika halafu ndio wakajenga kanisa lao, sasa uelewe maana yake ni kuuwa ukristo wa kweli na yake ya uongo mafundisho ya mpinga kristo ndiyo yakastawi mpaka ulimwengu wote. Akaniambia pia na Mtume Paulo na yeye alisema kweli aliwaonya wasiabudu sanamu na kubadilisha Neno la MUNGU, walichokifanya walimkata Paulo kichwa na mwili wake wakauzika halafu wakalijenga kanisa lao. Sasa nikuulize ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron hata kibinadamu umeshaona kanisa linawaua watumishi wa MUNGU? Jibu, hakuna. Na kama hilo kanisa analiongoza YESU WA NAZARETI aliyemtuma Petro au Paulo, je kanisa hilo lingemuua? Jibu, kanisa  hilo lisingemuua.
Kila mtu anajua kuwa Petro ni mwanafunzi wa YESU wa kweli kabisa, sasa kama Petro ni Mtume wa YESU je kwa nini hilo kanisa limpinge mafundisho yake? Au Mtume Paulo kwa nini alikatwa na kichwa? Ni sababu walipambana na mpinga kristo ambaye ndiye aliyeliteka kanisa sasa 98%. Sasa watu wote katika ulimwengu huu muokoke tena wokovu mtakatifu na muifuate kweli 100% kama kina Petro ndipo mtakuwa wanafunzi wa YESU. Mpaka hapa umeelewa sasa jinsi mpinga kristo alivyofanya na akafanikiwa kuuteka ulimwengu. Ila nawaeleza sasa hivi mpinga kristo hana nguvu tena ni wakati wa YESU sasa kuwavuna watu waende kwake na watoke katika kambi za shetani au makanisa yaliyo malango ya kuzimu sasa. Na kazi hii ni YESU WA NAZARETI ndiye anayeifanya peke yake kwa jinsi ajuavyo yeye peke yake. Hivyo ufunguke na uelewe inawezekana umejiona ni mkristo safi kumbe upo katika kambi ya shetani sasa ufunguke ufahamu wako na uwaeleze na wengine ili wapone.
NOTE:
Sasa kama Petro mwanafunzi wa YESU Waroma walimuua kwa sababu alikataa wasiabudu sanamu na kwenda kinyume na biblia na amri za MUNGU, je hamuoni wakristo mnaojiita wakristo, mnaoabudu sanamu mmekua mmeungana kumuua Petro kipindi kile au Mtume Paulo, kivipi? Kwa sababu, wao waliitetea injili ya kweli ya YESU WA NAZARETI walikataa injili ya yesu wa uongo! Kama unashiriki hayo na wewe ni mpinga kristo unampinga YESU WA NAZARETI aliyewatuma Petro na Paulo na sasa wako mbinguni.
MAKANISA AMBAYO NI MALANGO YA KUZIMU 100%
1.     Makanisa yanayoabudu sanamu.
2.     Makanisa ambayo yanabatiza ubatizo wa maji ya kikombe (ubatizo usio ubatizo wa Yohana yaani uliotoka mbinguni).
3.     Makanisa ambayo watumishi wanafananishwa na MUNGU au kuabudiwa.
4.     Makanisa ambayo viongozi wake ni wanachama wa freemason.
5.     Makanisa yenye benki au SACCOS au yanayofanya biashara
6.     Makanisa yanayofungisha ndoa za jinsia moja.
7.     Makanisa ambayo yanafungisha ndoa kwa agano la shida.
8.     Makanisa ambayo yanachangisha pesa katika kanisa, harambee.
9.     Makanisa ambayo watumishi wake (Wachungaji, Askofu na wengineo) hawajabatizwa ubatizo wa Yohana (siyo wanafunzi wa YESU wa kweli, ni wanafunzi wa yesu wa uongo ndio maana wamebatizwa ubatizo ambao YESU wa kweli hajabatizwa). Na makanisa yenye misalaba ambayo huichukulia ndiyo YESU au ndiyo Kristo.
10.  Makanisa ambayo yanabatiza watoto wadogo na kubariki watu wazima.
11.  Makanisa yote yenye partners na kuzika majina ya watu makanisani na biblia, na kupaka waumini majivu usoni.
NOTE:
Hiyo ni kazi yako wewe ujichunguze uko wapi, yamkini ulikuwa hauelewi sasa elewa toka huko, huko ni kwa shetani 100%. Wala usiogope lolote, roho yako ipone. Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo ninakueleza yanaonekana kwa macho ya mwili ila yapo mengi sana yaliyofichika rohoni ambayo ni mpaka MUNGU akufunulie peke yake kama alivyonifunulia na kunituma kwa watu wote na mimi hakuna atakayeweza kunizuia sababu kanisa la mwisho lenye nguvu limejengwa ndani yangu.
YESU ameingia kazini peke yake na nawaeleza watumishi mliofikiri kwamba kazi yake haitaenda mkamsaliti mkawa wachawi, freemason na kumuasi yeye na kuifuata miungu ya baali, japo midomoni mwenu mnalitaja jina la YESU ila ndani yenu ni mbwa mwitu. Ameniambia YESU mtaonana na yeye kwa jinsi anayojua yeye mmebadilika mmekuwa wagerasi wa kuwatesa watoto wake, sasa anawaokoa peke yake na serikali ya mbinguni.
Kila mtumishi ajichunguze mwenyewe je anatenda kama YESU alivyoagiza, jibu unalo, kama upo kinyume huko ndipo kumsaliti YESU na kumbuka hasara za kumsaliti YESU ni nini? Tazama yule Yuda mwisho wake ulikuwaje? Japo YESU alijua atakayemsaliti na akasema, na hata leo anasema amesalitiwa na mamilioni ya watumishi japo hata hao mamilioni robo tatu yao wamejiita wala mimi siwajui wala sitendi kazi nao ni wameitwa na mpinga kristo. Ila hiyo robo pia 98% wamenisaliti wote mimi YESU WA NAZARETI katika ulimwengu wote wamebakia 2% tu ndio hawajanisaliti. Na mtumishi aliemsaliti tayari yeye anaongozwa na malango ya kuzimu na kuwapeleka watu kuzimu badala ya mbinguni. Japo atahubiri habari za mbinguni ili usifunguke, chunguza matendo yake. Wacha tubu.
NOTE:
Ili roho yako ipone usiabudu katika nyumba za ibada ambazo ndio malango ya kuzimu, abudu katika kanisa ambalo hakika ni kanisa la mlango wa mbinguni kukufikisha na kukupeleka mbinguni alipo YESU WA NAZARETI. Chunguza mwenyewe hakika hautabisha japo wengine wanajikausha tu wamebakia na aibu. Neno la MUNGU ni upanga ndilo ilo linakata na linaponya, rejea kwa YESU.

OMBA TOBA:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU UNIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIONDOE KATIKA MAKANISA AMBAYO NI MALANGO YA KUZIMU, NIONGOZE KATIKA KANISA LILILOMLANGO WA MBINGUNI, NA NENO HILI LISITOKE MOYONI MWANGU
AMEN.
NAKUFUNIKA KWA DAMU YA YESU WA NAZARETI ALIYE HAI HATA SASA. SOMA KITABU CHA MPINGA KRISTO KIPO KANISANI KWANGU NA PIA KATIKA BLOG YANGU.
NABII HEBRON.

[ad_2]