IBADA YA MAJIVU NI IBADA YA CHAPA 666 (UFUNUO 13:16-18)

[ad_1]

IBADA YA MAJIVU NI IBADA YA CHAPA 666
                                                                                               UFUNUO 13:16-18
Naye atawafanya wote wadogo kwa wakubwa na matajiri kwa maskini na walio huru kwa watumwa,watiwe chapa katika mkono wao wa kuume  au katika vipaji vya nyuso zao. Hapa ndipo penye hekima , yeye mwenye akili aihesabu  hesabu ya mnyama huyo, maana ni hesabau ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita sitini na sita.

Ndugu msomaji haya yote yameshatimia ila yalikuwa yamefichika, na sasa MUNGU amenifunulia haya ili wanadamu wapone na wajue jinsi sasa shetani alivyojiingiza katika kanisa kwa kivuli cha jina la YESU.

Nitaeleza kidogo kuhusu hii chapa ya namba 666. Watu walifikiri itakuja namba kamili halafu mtu uandikwe usoni kwako, sivyo maana kila mtu anaogopa hiyo namba na haitaki isipokuwa wale ambao ni wapenzi au watoto wa shetani tu.

Jambo la kwanza unatakiwa ujiulize wewe mkristo, je ni kitu gani unapaswa kujipaka katika ibada yeyote, jibu ni damu ya YESU tu, na siyo majivu ya aina yeyote, na hata Biblia tafuta hakuna mahali wakristo tumeambiwa tupake majivu usoni na iwe ni ibada.

Alichoniambia YESU waambie watu wa ulimwengu, huo sio mpango wa MUNGU watu wapakwe majivu na kufanyika ibada hizo. YESU ameniambia hiyo ni namba 666 na siku hiyo au kila inaporudiwa na watu,  kupigwa chapa ni wanarichargiwa tena ili wasipotee katika ufalme wa shetani. Jiulize kwa nini wewe upakwe majivu? Hata kibinadamu mtu akipakwa majivu anakuwa kama shetani na anatisha kabisa, je wakristo hayo ndiyo mafundisho aliyotufundisha YESU wa Nazareti ambaye ndiye njia ya  uzima na ukweli? ( Yohana 14:6) usidanganyike YESU muda wowote anarudi, sisi hatujui muda,siku wala saa, usishiriki ibada hizo akija YESU hatakuchukua maana tayari unayo alama ya shetani tena bila ya wewe kujua ,nenda kokote na ubatizwe ubatizo wa maji mengi ili hiyo chapa ifutwe kwenye paji la uso wako na uwe huru umkimbie shetani na mawakala wake, mara nyingi YESU wa Nazareti amekuwa akisema na mimi na kunisisitiza waambie watoto wangu kwa sauti ya uchungu, waambie ukweli, wanirudie mimi BABA yao, maana watumishi nilio watuma wamenisaliti wameamua kumfuata shetani na ndiyo sababu watoto wake wanateseka, ila ole wao. Ameniambia Hebron,  makao niliyokwenda kuwaandalia watoto yapo tayari ila watu ni wachache, nikirudi kuja  wakati wowote nyumba nyingi zitakuwa hazina watu.

Wengi ni wa shetani 98% ya watu wote wa dunia hii, ewe mwanadamu maneno haya siyo  yangu mimi Hebron. Ni ya YESU wa Nazareti aliyoyatoa katika kinywa chake, uyafanyie kazi na wewe utapona.

Kupakwa majivu na mafuta  huko ni kupigwa muhuri wa namba 666 soma ( Ufunuo 13:16-18) na wewe utakuwa huru. Usidanganyike tena na usishiriki tena kama unataka kwenda mbinguni na zaidi hao wanaowapaka majivu, hao wapo kinyume na Biblia isemavyo na zaidi hayo hayapo katika kitabu cha MUNGU yani kitabu kitakatifu, na ukisoma katika kitabu cha ufunuo wa Yohana (22:18-20) ole wake atakayeongeza mafundisho tofauti, Jehanamu inamsubiri.

NABII HEBRON

[ad_2]