Close

KIBALI CHA MUNGU KWAKO.



Normal
0

false
false
false

EN-US
X-NONE
X-NONE

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:8.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:107%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,sans-serif;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}

Nawasalimia katika jina la YESU

Tuombe Baba katika Jina la YESU
nawaombea watoto wako nguvu ya kupokea neno na kulitendea kazi Naangusha falme
zote na mamlaka zote  za giza katika Jina
la YESU, Bwana  YESU anawapenda na
anataka kuwafundisha kuhusu kibali.

Neno la MUNGU linatoka katika
kitabu cha Matendo 10:35-36, Napenda ujue mwana wa MUNGU utendaji kazi wako
utapimwa , maisha hayatafanana na mbinguni, itapimwa jinsi ulivyofan nv d   ya
kazi ya MUNGU huku duniani mfano unaomba kwa dakika tatu kwa wiki itapimwa,
alivyokupa MUNGU siku ya mwisho yatapimwa, utowaji wako utapimwa,
unavyohudhuria vipindi utapimwa maneno haya ninayoyasema ya sikilize hata siku
ya mwisho yatakuwepo wako malaika wanaoangalia rekodi yako kila siku MUNGU amekuwa
akisema na mimi sana kuhusu kibali, tunaona yakwamba kaini uso wake
ulikunjamana kwa sababu habili ndugu yake alipata kibali kwa MUNGU kwa sadaka
yake, lakini kaini hakupata kibali jambo hilo likamchukiza sana Kaini,kuna aina
mbalimbali za kibali,kuna kibali umepewa na 
MUNGU, kibali umepewa na miungu, kibali umepewa na majini, kibali cha
mizimu, pia kuna kibali umepewa na wanadamu mfano, kibali cha kuendesha gari
ambacho kinahakikishwa kwamba wewe unafaa, watu wengi leo hii hawana kibali
kama kaini,kwa kujua na kutokujua, Habili alikuwa na kibali mbele za MUNGU ndio
maana sadaka zake zikapokelewa,sadaka zake zikafika, kaini hakuwa na kibali
mbele za MUNGU kwa sababu alitenda mabaya, hata leo hii kuna watu hawapokelewa
sadaka zao mbele za MUNGU kwa kujua na kutokujua lakini nataka nikufundishe ili
ujue ukapate kibali mbele za MUNGU kwa jua na kutokujua lakini nataka
nikufundishw ili ujue ukipata kibali mbele za MUNGU,  Tunaona alisema hakika  MUNGU hana upendeleo ukitenda haki mbele za
MUNGU utapata kibali, kuna watu leo hii wanasema MUNGU ana upendeleo, MUNGU hana
upendeleo jiangalie wewe kwanza tenda mema kwake utaona kibali, lakini dunia
hii unaweza ukawa unakubalika na watu wenye nguvu za giza siyo kibali cha
MUNGU, watu wengi hawana kibali mbele za MUNGU,wewe kama huna kibali mbele za
MUNGU ni sawa kama umekufa  huwezi kuwa
na chochote katika dunia hii.

 

Kibali ni Roho ambayo MUNGU anawapa
wanadamu, leo hii watu wanataka kibali mbele ya wafalme, mbele ya mtajiri
badala ya kutaka kibali mbele za MUNGU, ukipata kibali mbele za MUNGU, MUNGU
anafanya kibali katika mambo yote kwenye dunia hii, kiko kikabli cha wokovu
ndicho kibali kitakachokupeleka mbinguni 
lakini watu siku hizi wanakatazwa kuokoka nausipookoka hauwezi kufika
mbinguni lazima uokoke, kuna kibali na  Neema
watu wengine kwa sababu ya kutenda mabaya neema inapungua mpaka kibali
kinakwisha, Bwana YESU asifiwe! Nitasoma kitabucha Esta sura 5:2, Esta alizaliwa
na neema ya kibali cha MUNGU, laikini kuna wakati mambo yalikuwa magumu
waliamua kuomba kibali kwa MUNGU kwa MUNGU hawakuomba kwa mfalme, mfalme  akageuza kila kibali kwa mfalme, mfalme
akamnyenyekea Esta kwa sababu MUNGU alimpa Esta Kibali, Bwana YESU asifiwe!
Sana kuna mtu atakuwa anaomba kibali kwa kiongozi wa kanisa badala   ya kuomba kibali kwa MUNGU watu hawataki
kutafuta uso wa Bwana wapate kibali, wakristo wengi hawana kibali cha kwenda
mbinguni, hawana kibali cha kuwa karibu na Bwana Yesu mbinguni wanakwenda wenye
kibali na Biblia  inasema lazima ulinde
neema ulinde kibali hicho,hutakilinda kwa Rungu utakilinda kwa maombi.

 

Yawezekana kibali chako wewe ni cha
kukataliwa,kuchukukiwa, kudharauliwa na hapo ndipo utaona dunia ni chungu
kwasababu ya mateso kwa sababu huna kibali cha MUNGU, Nyakati zile za mwisho
kitaondoka kibali cha kutubu,kitaondoka kibali cha kulielewa neno hata ukisoma
hutaelewa,  Biblia  ndivyo itakavyokuwa, bali wale wenye neema na
kibali cha MUNGU ndio watakaoelewa hata sasa watu hawaelewi neno la MUNGU bali
wanaelewa uongo.

Bwana YESU asifiwe! Ukiwa na kibali
cha MUNGU hakuna kitakachokuweza angalia 
mfano wa Esta alikuwa na kibali kwani walimuweza? Hapana Soma Mwanzo
39:21 Yusuphu alizaliwa na neema ya kuwa waziri mkuu na yeye alielewa namna ya
kutafuta kibali za Bwana, angalia mfano wa Yusufu alivyopata kibali mbele ya
mkuu wa magereza, Mkuu wa magereza alikuwa hamjui yusufu lakini kibali cha
MUNGU ndani ya Yusufu kilimfanya Mkuu wa magereza ampe Yusufu kibali. Na hata
wewe shetani anajua kabisa wewe utakuwa nani kwa Kibali cha MUNGU alichokuwekea
Ndani yako lazima atakuwekea  usiku, inabidi
uombe kibali mbele za MUNGU.

Inawezekana umeolewa lakini kibali
na Neema ya ndoa imechoka unakosa kibali kwa mume wako, umekosa kibali kwa mke
wako, yawezekana  ni mtumishi, Mchungaji
yakupasa uombe kibali machoni pa Bwana, yawezekana ni muimbaji yakubidi kuomba
kibali mbele za MUNGU lakini shida iliyoko watu hawataki kuomba kibali mbele za
MUNGU, yawezekana unafunga sana na kuomba lakini huna kibali mbele za MUNGU
mambo yatakuwa Magumu, mkiwa na kibali mbele za MUNGU  hata wachawi wanakuloga vipi.

 

Mambo yako yatakuwa shwari
hawatakuweza, kama yaliyomtokea Yusufu alitaka akalinda neema yake kwa kutafuta
uso wa MUNGU. Sasa kuna watu ambao MUNGU anawatoa kwenye ulevi anawapa uwezo wa
kushuhudia lakini kama huna kibali cha MUNGU watu bado watabaki na mafaili ya
ulevi wako wa zamani, kwa hiyo chochea hiyo neema hata mimi sasa hivi nina hubiri
lakini watu bado wako na mafaili ya zamani, lakini nimechochea kibali ambacho
MUNGU amenipa ndio maana leo mmejazana, Haleluya!

 Inawezekana ni mfanya biashara, MUNGU amekupa
kibali hicho, au karama ya ukulima inyenyekee kumuomba MUNGU kibali ili
akuongezee Ekari za kulima, watu wmechoka kwa sababu neema aliyokupa pengine ni
Uinjilisti au amekupa Udaktari, au fundi, amekupa kumpigia makofi, amekupa
neema ya kumtumikia na mali zako unatakiwa uombee kibali ndipo mambo
yatafunguka lakini ukikaa na kusema mimi ni mtoto wa mfalme ‘’my friend’’ mambo
yatakua magumu unaweza ukabadilishiwa neema yako ukawekewa neema ya kishamba tu
ukawekewa Uwoga, kinachotakiwa kuomba neema ya kuvaa vizuri, neema ya ujasiri,
unaweza ukawekewa neema ya kuvuta bangi tu, kuvuta sigara tu inakubidi uombe
kibali cha kuokoka, na ukishaokoka ombea wokovu wako kibali ili wasikuweze kama
walivyotaka kufanya kwa Esta ikashindikana, walivyotaka kufanya kwa Ayubu
ikashindikana – Bwana Yesu asifiwe!

 

        Sasa unapoitunza neema sana ndipo
unaenda kupata kibali sana, soma kitabu cha Samueli 1;2:26, leo watoto wengi
wanazaliwa kwa neema lakini hawana vibali kwa Bwana lazima umuombe kibali kwa
Bwana, Sunday School humpeleki, unmpeleka Baa tu, mtoto atajifunza vitu vya Baa
tu atajifunza mambo ya MUNGU saa ngapi, 
Hata YESU mwenyewe alipoulizwa na wazazi wake pale walipokua wakimtafuta
aliwajibu inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu alikua na kibali cha
kwenda nyumbani ka Bwana, Sasa kama huna kibali cha kuhudhuria Ibada, huna
kibali cha kuhudhuria mikesha itakuwaje inabidi uombe kibali.

 

            Inawezekana na wewe hapo MUNGU
ameweka kitu ndani yako lakini unakikalia tu, kwa sababu huna kibali mbele za
MUNGU na mbele za madhabahu, inakubidi uombe kibali ili uwee kuvifanyia kazi na
MUNGU atakuinua – Soma Waebrania 12:15 kwa hiyo kila mtu ana neema ya MUNGU
ikikupungukia hutaenda mbinguni, ikikupungukia hutaweza Vita, hata malaika
walikua na neema ya MUNGU lakini ilipowapungukia waliitwa wana wa shetani
angalia na wewe neema ya MUNGU isikupungukie usije ukaitwa mwana wa shetani.
Bwana YESU asifiwe! Angalia Daniel alikua na kibali mbele ya macho ya MUNGU kwa
hiyo walipomuweka kwenye tundu la simba hawakumdhuru kwa kuwa alikua na kibali
mbele za Baba yake hata wakati amechoka alirudi kwa Baba yake kuomba kibali
ndipo aliposhuka Elia na Musa kumtia nguvu hicho kilikua kibali cha MUNGU ndani
yake kibali ni Roho lazima uombe, ngoja nikwambie hakuna maisha magumu katika
Dunia hii kama kukosa kibali mbele za MUNGU. Inawezekana wewe unayo neema ya
kua mtu fulani lakini kwa kua hunyenyekei ujue hilo jambo halitatokea itabaki
historia nilikuaga,Shetani hapendi watu kupata kibali toka kwa MUNGU ili mambo
yao yanyooke shetani amewafunga Shetani amewafunga kabisa, hivi MUNGU akiweka
kibali mbele zako hata majaribu yanapokuja utayaona takataka.

 

           Mnaweza mkawekwa Magerezani, mnaweza
mkasingiziwa lakini mnapaswa kushikamana Shetani akikukosa kwenye Uchawi kwenye
nini anakutafuta neema iondoke lakini mkishikamana hamtawezwa. Unashikamana
kiroho mnashikamana kimwili, mfano wa yule mwanafunzi mmoja alimkata sikio
mlinzi mmoja wao kwa sababu walikuwa wameshikamana na Bwana YESU.

 Haleluya! Leo hii ukiona mwenzako ameanguka
kwenye wokovu mnawatema mate, Bwana YESU alikuja kwa ajili ya wenye dhambi na
ndipo ataokoka, sio wewe uwe na kazi ya kumhukumu mwingine, jichunguze wewe
umetenda mangapi, jifunze kuteteana kama Bwana YESU alivyokuja duniani kufanya
kazi ya wokovu, kuwaokowa watu usimseme mtu mwenye kibali cha Bwana
utaharibikiwa, Mtumishi akiwa na kibali cha Bwana atahubiri kweli, Ukiwa na
kibali cha Bwana huwezi kuabudu sanamu kama MUNGU ukiwa na kibali cha Bwana
huwezi kuombea mtu kwa kutoza pesa, hivyo ni vibali vya shetani hawana huruma,
ni afadhali ukienda Hospitali watakutibu ili usikate roho watakwambia ulipe
pesa baadae lakini kwa mtumishi mwenye kibali cha shetani atataka pesa kabla
kumuombea mtu ata kama anakata roho ni mpaka atoe pesa, Nabii Hebron nina
kibali cha kupeleka watu mbinguni nina kibali cha kuponya bure, sina kibali cha
mapooza, sina kibali cha kigeugeu, nina kibali chako nina kibali cha mataifa
cha kukuongoza ufike mbinguni. Haleluya! MUNGU amewaletea kibli cha ubatizo wa
maji mengi nyie mnataka ubatizo wa kisima, wa kikombe alafu unaenda mbele za
MUNGU atakwambia kwenda wewe, inawezekana una kibali cha kwenye masanamu YESU
hakanyagi huko hata kama unalitaja jina la YESU, ninakuambia uombe kibali cha
kwenda mbinguni ukiwa hai hautapata kibali cha kwenda mbinguni ukishakufa eti
unaombewa na watu ukiwa kaburini hutaenda mbinguni ukisha kufa ndio uende
mbinguni ni uongo. MUNGU wetu sio wa wafu MUNGU wetu yu hai anaongea na walio
hai, bali wanaombea wafu wanamuomba MUNGU mfu.

 

 Mtu asiye na kibali cha MUNGU ni mtu
anayesahaulika ni mtu hata hakumbukwi unaweza ukakosa hata kibali cha pesa,
unaweza ukakosa kibali cha chakula, unaweza ukakosa kibali cha mavazi, unaweza
ukakosa kibali cha kusalimiwa hata kukumbukwa, 
MUNGU anasema amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu, mtegemee yeye lakini
watu wamebadilika wanamtegemea mwanadamu kwa akili zao za kinafki kwa mfano mtu
anakukumbuka siku mtot amelazwa Hospitali ili umpe pesa ya kumtoa mtoto, kuna
mtu anakukumbuka saa anafukuzwa kwenye nyumba, hivi ni vibali vya shetani.

 Kibali kinalindwa kwa maombi mfano Esta
aliangalia ahadi ya MUNGU akaomba kibali tazama walikua waangamizwe lakini
kibali kiliondoa, angalia Sara alikuwa na neema akatembelewa na malaika kupewa
habari za kupata mtoto uzeeni Sara alicheka alijidharau kwa umri alio nao,
yawezekana hata wewe unaambiwa utapata Gari unajidharau ukiangalia hali
uliyonayo, Ibrahimu kabla ya kuzaliwa alikuwa na neema ya kuwa Baba wa mataifa
na ikawa, kwa hiyo wewe ndiye utakayesababisha alichokupa MUNGU kitokee.
Sulemani alikua na kibali cha kumjengea MUNGU lakini Baba yake Daudi hakua na hicho
kibali ila angeomba angelipewa.

 

Kibali kinaweza kuibiwa ili
kisiibiwe unakitolea sadaka ya ulinzi, familia inaweza kukunenea hutapata mtoto
na kweli hutapata mfano hutaishi na mke na kweli hutaishi na mke, lakini
ukiomba kibali hayo hayatatokea, kuna kibali cha kukaa na mke wako, kuna kibali
cha kuja madhabahuni kama vile Samueli, kama kikichukuliwa huji,kun ahata  kibali cha kumshangilia MUNGU.

 

 Kibali chako kikichukuliwa unakuwa mtu wa
kukata tamaa unaona hupendwi, unaanza kua mtu wa hasira unaanza kuwa mtu asie
na maisha mazuri, ukiona hivyo omba kibali kwa MUNGU, ukipata kibali utaona
mambo ya ajabu, kama wewe ni mwan ndoa kibali la sivyo mtaishi maisha kama ya
mbuzi na kondoo, kama sio watu, ni mchungaji omba kibali ni muimbaji omba,
unaweza kuwa na kibali cha kukata tamaa tu, unaweza ukawa na kibali cha kwenda
kuzimu na unakwenda kuzimu, kama una mtoto muombee kibali cha MUNGU
asitumikishwe na wachawi, mwombee kibali cha kuja hemani mwa Bwana, watoto wana
vibali vya pombe, vibali vya Bangi kwa sababu mama yake alivyokua mjamzito alikuwa
akitumia vitu hivyo, Omba kibali cha utajiri omba kibali cha cheo, omba kibali
cha kusoma, omba kibali cha kuheshimika, kibali cha kupenda watu, kibali cha
kuheshimu watu, Vibali vya watu wengi vinashikiliwa na ukoo, kuna watu hawana
ata kibali cha kwenda Nchi za nje kuna watu hawana kibali cha kuambatana na
wenzi wao, wengine hawana hata neema ya kucheka na wake zao, neema ya kufunga
ndoa omba kibali.

 

Kibali kinaendana na Nyota, kuna
kibali cha kung’ang’ana na Bwana YESU, kibali kinaweza kuisha muda, ukikosa
ibada mara nyingi kibali kinaisha au kupungua kuna kibali cha Roho Mtakatifiu,
ukiwa na kibali mambo yako yanakua rahisi, kuna kibali cha miaka yako, kuna
kibali cha kumsujudia MUNGU, kuna kibali cha kupiga magoti, kibali cha
kunyenyekea MUNGU, kibali cha ulinzi omba kibali cha kazi ya mikono yako,
kibali cha kusogea madhabahuni pa Bwana. Vibali vyako vitarudi kwa njia ya
maombi.

 

Sema Bwana YESU asante kwa neno
lako niko mbele zako ndani ya agano la Damu ya YESU naomba toba rehema na
msamaha kwa yote niliyokosa kwa mawazo, kwa maneno, na vitendo vyote vya uovu-
nakukubali wewe kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yangu, namkataa shetani na
mambo yake yote futa jina langu kwenye kitabu cha hukumu, andika jina langu
kwenye kitabu cha uzima wa milele – 
Bwana YESU nakuomba unirejeshee vibali vyangu vyote vilivyochukuliwa na
adui kama upendavyo Amen!

 

Prophet hebron Wilson kisamo.