[ad_1]
Ndoa zote za kufunga na mimba kwa wakristo, hizo sizo ndoa za mpango wa MUNGU, hizo ni ndoa za uzinzi au mshahara wa dhambi , au matunda ya shetani halafu mnamshirikisha MUNGU na kusema eti ameunganisha yeye. Huo ni uongo mtupu hata nyie mnaofungiwa nawaeleza hata ripoti za majina ya ndoa zenu hazipo katika kitabu cha ndoa mbinguni.
Na laumu siyo ya waumini, mngeambiwa ukweli msingezini, ila kwa sababu ya maadili mabaya ya makanisa ya sasa yaliyoacha njia ya MUNGU, na pia hofu ya MUNGU imeondoka kwao wamekuwa na roho ya kuasi na kuzibariki dhambi makanisani, kwa waumini mkawa na mimba.
Hivi inaingia akilini kweli,? eti MUNGU atabariki kazi za shetani? Jibu ni haiingii akilini, na kama haiingii akilini je ni kwa nini sasa watumishi wanaruhusu kufungisha ndoa hizo? Jibu, hata wao ndani ya mioyo yao hofu ya MUNGU haipo tena ni roho ya kuasi kabisa.
Tena wanamtaja ROHO MTAKATIFU na BABA na MWANA katika kuubariki uzinzi, ukweli ni huu, haijalishi harusi imefungwa kwa gharama gani, uwe umebeba mimba kabla ya ndoa(harusi) hilo ni tunda la dhambi na mtoto atakuwa na hiyo roho ya dhambi ya uzinzi ambapo alipatikana katika njia hiyo.
Apandacho mtu ndicho avunacho. Na hata wanaofungisha ndoa hizo tena binti anaonekana tumbo kubwa anaingia kanisani bila aibu na eti YESU anaunganisha huo uzinzi?
Ndoa hizo hazija unganishwa na YESU WA NAZARETI . wala hazina baraka za MUNGU. Hii inamuhusu binti aliyebeba mimba , na kijana aliyemzinisha na pia dhambi hii inamuhusu mtumishi aliyeruhusu kumfungisha au kuhalalisha dhambi hiyo na pia dhambi hiyo ya uzinzi inalikamata kanisa lote.
Maana alivyo kuhani na afanyavyo ndivyo na kanisa lake. Je, ndivyo MUNGU awaagiza hivi? Soma amri 10 za MUNGU ! je, haijavunjwa (Usizini) halafu eti huyo huyo MUNGU awe kigeu geu aukubali uchafu huo na aubariki? Je , ni kweli ? msidanganyike, acheni uzinzi tiini mpango wa MUNGU.
NOTE:
NDOA ZOTE ZA JINSI HII HAZIPO KATIKA KATIKA KITABU CHA NDOA ALIZOZIFUNGA MUNGU. Na hajazifunga yeye na hazina baraka za MUNGU, wala mkono wake haupo juu yake, na ndoa zote zinazofungwa kwa agano la shida au laana na raha, MUNGU halaani, ndoa anazozifungisha baali anazibariki, na wewe kwa kuwa umekiri shida na raha, shida itakufuata milele, shida ni roho na hukua mahali ilipo kubaliwa kama watu wanavyozikiri katika makanisa kinyume na mpango wa MUNGU.
UFUNUO 22:18 -20
Tazama Rebeca alibarikiwa tuu na hakulaaniwa Mwanzo 24: 56-61.
NABII HEBRON
[ad_2]