[ad_1]
Enyi mataifa yote, nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI, anawapenda sana amenituma niwaeleze habari zake ili umjue yeye kikweli 100%. Leo nitawafundisha habari inayohusu (pepo mhubiri). Pepo huyu anatoka kuzimu kwa yesu wa uongo katika kitengo cha injili ya uongo ili kuwapotosha mataifa wasiende mbinguni, kazi yake ni kuhubiri na kuwapa nguvu za kipepo watumishi na kulibadilisha Neno la MUNGU aliye hai na kulifanya kinyume mfano soma katika kitabu cha Wagalatia 1:1-16. Katika vitabu vyake vya injili shetani anacho na yeye kitabu chake cha uzima wa mauti ya milele ambayo ndiyo biblia ya kuzimu, na ina kitabu cha kwanza mpaka cha mwisho, ila yaliyopo ndani ya biblia hiyo yamebadilishwa na kuwa kinyume na maneno ya MUNGU aliye hai na katika ulimwengu huu hicho kitabu halipo kimwili wala hauwezi ukakipata ila jinsi kitabu hiki kinavyopatikana shetani hutuma huyu pepo kwa watumishi na anaingia ndani yao na akishaingia tu mtumishi anabadilika na yeye anaanza kwenda tofauti na Neno la MUNGU, na hata ukimuuliza kwa nini unaenda tofauti na biblia utaona hana jibu sababu anayoyafanya siyo Neno la MUNGU lakini ndani ya kanisa utaona anasimamia kanisa kama kawaida au dhehebu na kumbe ilo analoliongoza sasa anasambaza roho za shetani zenye maandiko ya shetani ili kuziua roho za wana wa MUNGU katika uliwengu wa roho na roho zinakufa.
Mfano halisi hivi hamshangai wakristo baadhi yao katika makanisa wanabatizwa ubatizo ambao haupo katika biblia takatifu! Yaani ubatizo wa maji ya kikombe ukiona watu wanabatizwa ubatizo wa maji ya kikombe ujue wanapokea mapokeo yaliyopo katika kitabu cha uzima wa shetani wakaupokea mauti. Sasa elimu yeyote tofauti na ya biblia katika kanisa na ukafundishwa ukaipokea ujue umepokea uzima wa mauti ya milele. Nasema ni uzima wa mauti ya milele kwa sababu ukifa utahukumiwa na utachomwa moto milele na utayasikia maumivu ya moto milele (huo ndio uzima wa mauti ya milele). Pepo mhubiri jinsi anavyofanya kazi anawaletea mafunuo ya kipepo na humletea yule aliyemteka au kumletea mafundisho ya kipepo yule ambaye anafanya kazi ya utumishi kwa njia ya uchawi au amejiita au amejifanya au aliyeitwa na MUNGU halafu akamuasi MUNGU au kumsaliti YESU. Kumsaliti YESU ni kulitamka jina la YESU lakini watu hawalitendi Neno la kweli, hao ni wanafiki, sasa watu hao ndiyo wanaongozwa na mapepo mhubiri ili kuwaua wanadamu roho zao.
HII NI MIFANO MICHACHE YA KUJUA MTUMISHI AU WATUMISHI WENYE PEPO MHUBIRI NA SIYO ROHO MTAKATIFU:-
1. Mfano kanisa lina benki ujue hilo kanisa lililopo ndani ya mtumishi huyo limejengwa na shetani na ndani yake pepo mhubiri ndiye anayehubiri kupitia kinywa chake na siyo ROHO wa MUNGU wa kweli, biblia haijaruhusu kanisa kuchaji riba, ila biblia ya uzima wa mauti imeruhusu hivyo. Hapo ni kuzimu, ondoka, ndani ya mtumishi huyo ni pepo mhubiri ndiye anayefanya kazi, na kama ni pepo mhubiri jiulize je kuna uzima wa milele hapo? Jibu unacho.
2. Mahali popote panapo batiza ubatizo wa kikombe au ukabatizwa na maji ya kisima au ukabatizwa kwa jina la mchungaji haijalishi imetajwa BABA na MWANA na ROHO MTAKATIFU au jina la YESU huo ni upofu wa kukupinga wewe ujione upo sawa sawa kumbe umeshauwawa kiroho na kazi zao zote ipo roho ya shetani inafanya kazi na siyo ROHO ya MUNGU wa kweli inayofanya kazi hapo, ukiona haya yanatendeka katika kanisa lolote sasa uelewe wanaongozwa na pepo mhubiri na mamilioni ya wakristo wanajiona wapo katika nuru bali ukweli wapo katika giza. Hili ni giza la kuzimu wanaowekewa watu ili wasimuone MUNGU na wasiende mbinguni.
3. Watumishi wote ambao ni wanachama wa freemason, wachawi, wafufua misukule, wanaotoa vitu vya aina yeyote ndani ya miili ya binadamu mfano mawe, nywele, nyoka, miiba, kijiti na vinginevyo hao wote wanaongozwa na pepo mhubiri na yeye ndiye anayeitenda hiyo miujiza ya kipepo au kimazingaumbwe.
4. Watumishi wanaowahonga watu pesa waseme shuhuda za uongo katika makanisa yao, watumishi wote wazinzi, walevi, waabudu sanamu na wanaopinga wokovu, wanaofanya ibada za wafu, hao wote ndani yao yupo pepo mhubiri siyo ROHO wa kweli wa MUNGU, ingekuwa ni Neno la kweli kama ilivyo katika biblia hapo ROHO atakaa ila ikiwa ni tofauti hapo ni mapepo mhubiri ndiyo yanaishi.
5. Kuabudu sanamu, kuabudu watoto wa MUNGU na kuwajengea sanamu, hapo ni pepo mhubiri ndiye anayeongoza ili awape watu uzima wa mauti ya milele na wote wanaoshiriki hayo wao wanayo tiketi tayari ya uzima wa mauti.
6. Makanisa yanayofanya harambee, kufanya michango ndani ya nyumba ya sala, kuchoma ubani (ubani ni chakula cha majini). Kuandika sadaka majina na kupewa risiti. Kanisa linalosoma ripoti ya matumizi kwa waumini badala ya viongozi kumshirikisha MUNGU peke yake, inakuwa tena hiyo siyo sadaka, kwa MUNGU, bali inakuwa kama ni kampuni watu wanasomewa matumizi ya pesa walizozitoa kuendeshea kampuni. Ukitoa sadaka umempa MUNGU au siyo? Sasa ukimpa MUNGU unamuuliza eti unafanyia nini pesa yangu? Ukiona hivyo ujue pesa zenu hazijaenda kwa MUNGU ila zimeenda kwa shetani ambaye ndiye aina ya mungu pia, sasa hii ni kazi ya pepo mhubiri.
7. Kanisa lenye partners hawa wote wanaibiwa pesa zao na pepo mhubiri maana YESU hana ubaguzi, sababu mojawapo hata wewe ufikirie kwa nini siku zote partners lazima wawachague wenye pesa tu? Je kama kweli ni ROHO ya MUNGU wa kweli inawabagua wasio na pesa? Huu ni unyang’anyi na kazi hii inafanywa na pepo mhubiri na ni pepo hawa wapo ndani ya watumishi waliomsaliti YESU. Sasa somo umelielewa, partners ipo katika biblia ya uzima wa mauti ila katika biblia ya uzima wa milele imeandikwa mtumishi usisumbukie utakula nini utavaa nini, kama mimi MUNGU ninayanyeshea maua je wewe mtumishi wangu si bora zaidi? Sasa uelewe sababu siyo ROHO wa MUNGU anafanya kazi ndani ya mtumishi ni pepo mhubiri ndiyo maana anafanya hivyo ili shetani aiendeleze kazi yake na kuujenga ufalme wake zaidi kama ilivyo sasa. Ulimwenguni mwote jina la watumishi na makanisa yamenuka hii ni sababu ya jini mhubiri na makanisa yanatenda uovu, mabaya sababu ROHO wa kweli wa MUNGU hayupo yanayotendewa hapo ni ya shetani.
8. Watumishi wote wanaotoa stika, vitambaa, vilemba, kalenda halafu wanakueleza utembee nazo zitakulinda na wengine wanatoa kalamu. Hawa wote ni wachawi 100% wanaongozwa na pepo mhubiri.
9. Mtumishi yeyote ukiona anataka kwenda kuhubiri halafu anachangisha pesa za kwenda kuhubiri, ujue huyo hajatumwa na MUNGU, maana yeye angetumwa na yeye, yeye peke yake angemuandalia njia ya kwenda, ila sababu hajatumwa na MUNGU huko ndani yake yapo maneno ya shetani na pepo mhubiri formula yake ni mchango. Hata kama ni kuchangisha pesa kwa ajili ya vipindi vya Television, radio hata kununua gari la mtumishi akichangisha tu ujue huyo analo pepo mhubiri ndani yake. Akiwa hana pepo mhubiri anao ROHO wa MUNGU peke yake MUNGU atafanya peke yake. Imeandikwa usimtegemee mwanadamu, huku ndipo kumtegemea mwanadamu na lazima wafanye hivyo maana formula ya shetani ni kumtegemea mwanadamu na ndivyo ilivyoandikwa kwenye biblia ya shetani.
10. Kanisa lenye sadaka zaidi ya sadaka ya shukurani na fungu la kumi tu. Hizi mbili ndizo za kweli, hizo nyingine zote ni za biblia ya shetani na kanisa hilo lenye sadaka tofauti na hizi mbili hizo zilizoongezeka makanisani zimetoka katika biblia ya shetani, na kwa kufanya hivyo tayari mahali hapo ni pango la unyang’anyi. Mfano hakuna sadaka ya ahadi wala collect katika biblia takatifu ila katika biblia ya shetani nimeona hiyo sadaka ya ahadi na collect ipo. Sasa chagua leo yupi utakayemtumikia, toka huko ni pango la mapepo.
11. Jini mhubiri huyo anao manabii, wachungaji, wainjilisti, mitume, waalimu hivyo hivyo. Hivyo watu wakisikia manabii hawaelewi wapo wa aina mbili, hizi huduma tano zipo za aina mbili, zipo za MUNGU aliye hai na pia shetani na yeye anazo zake tano, ila utazitambuaje, ipi ni ya shetani na ipi ni ya MUNGU, chunguza matendo yao picha utaipata, chunguza kiroho na kimwili. Na 98% ya huduma hizi tano katika ulimwengu wote sizo huduma tano za MUNGU aliye hai ni huduma tano za shetani ambazo zipo chini ya jini mhubiri na malaika zake wa lusifa ambazo zipo ndani ya watumishi zinatenda kazi, uponyaji wa kipepo, miujiza ya kipepo, na katika biblia ya shetani, amefananisha biblia yake na majina yote ya walioandika biblia, mfano Yeremia, Daudi, Musa, Petro na wote walioandika biblia takatifu, shetani naye anacopy majina yao akaweka na sura hivyo hivyo. Ila amebadilisha vifungu vyote na jinsi inavyofanya kazi kwa watumishi wa uongo hapa ulimwenguni.
Utashangaa labda unafundishwa habari za Eliya au Elisha kibinadamu mtamuona anasoma biblia kimwili ila katika ulimwengu wa roho anasoma biblia ya shetani na yatafanyika maajabu ya kipepo kwa kutii yale mambo yanayoletwa na pepo mhubiri kama vile masharti. Pepo huyo mhubiri ndiyo pepo ambaye pia anafanya kazi za wanajimu au waganga wa kienyeji. Sasa siku hizi wapo manabii, mitume, wachungaji, wainjilisti, waalimu ambao ni wanajimu wa shetani, ila huku uliwenguni mnaona ni mtumishi wa MUNGU, mtawajuaje? Fuatilia mafundisho yao, utaona wanakazana na mafundisho ya baraka tu na utajiri. Sasa uelewe somo hili vizuri na usome makala ya Nabii Hebron utafunguka zaidi na roho yako itapona ukiyafuata mafundisho haya na kukuonya uache uovu. Ukikuta mtumishi yeyote anadai umpe pesa ndio ufunguliwe ujue huyo ndani yake yupo pepo, ni mganga wa kienyeji lazima utoe kitu kidogo ndiyo akupe msaada na zaidi haufunguliwi anakuongezea pepo lingine lipoozee tu, maana belzebuli hawezi kumfitini belzebuli mwenzake au ufalme mmoja hauwezi kuufitini ufalme huo huo ambao ni group moja.
NOTE:
Kama mtumishi unayetaka kupona tubu na unajijua unalo pepo mhubiri na utoke kabisa mahali ulipo na unafanya kazi hiyo ya shetani, yamkini ulikuwa haujui ila wengi wanajua haya ila amenituma YESU niyafichue haya na yule anayenichukia mimi hanichukii mimi ajijue anamchukia YESU, hata anayeniombea mabaya, ajijue anamuombea YESU mabaya na hatafanikiwa milele, YESU anarudi sasa okokeni. Kataeni mafundisho ya pepo mhubiri bali myapokee maneno ya MUNGU tu aliye hai na uyachunguze, ukikuta mnatenda tofauti na biblia takatifu hata jambo moja ujue siyo ROHO MTAKATIFU anayewaongoza ni pepo mhubiri au kristo wa uongo.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU MIMI NINA DHAMBI NAOMBA UNISAMEHE UNIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA NA WEWE YESU WA NAZARETI UWE BABA YANGU MILELE, NIPONYE ROHO YANGU, NIONGOZE WEWE PEKE YAKO, KWANZIA SASA NIFUNGUE NA FAHAMU ZANGU NIZIDI KUKUJUA WEWE.
NOTE:
Soma makala ya Nabii Hebron na vitabu nilivyoviandika vitatumika kukukuza kiroho huko ulipo au katika nchi uliyopo na zaidi karibu sana katika kanisa la YESU Tanzania, utakutana na YESU WA NAZARETI atakufungua, atakuponya na kukubariki.
Mlindwe na YESU WA NAZARETI
NABII HEBRON.
[ad_2]