[ad_1]
Nawasalimu kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI aliye hai na ndiye aliye mwana wa MUNGU wa pekee na mpaka sasa hajatokea kama yeye na hatatokea mwingine zaidi yake. Siku ya Pasaka 20.04.2014 aliniambia Hebron najua leo mnasherekea siku ya ushindi ambayo mnakumbuka nilipoteswa na kuzikwa na nikafufuka ili muwe huru. Akaniambia nakutuma kwa watu wote na mataifa yote uwaeleze kila mtu abatizwe ubatizo wa maji mengi kama nilivyobatizwa mimi katika maji yanayotembea, na pia waokoke na kuishi katika utakatifu siku zote, mimi nakaribia kurudi nitakuja kuwachukua wale tu waliobatizwa kwa ubatizo niliobatizwa mimi ambao ndiyo ubatizo wa MUNGU ambao pia ndiyo Yohana alianzisha hapa ulimwenguni na mimi YESU nilibatizwa hivyo hivyo, pia nitawachukua waliookoka na kuishi maisha matakatifu peke yake.
Kwa hiyo kila mtu ajichunguze je haya mambo matatu umeyatimiza? Na je unaishi katika maisha matakatifu? Au umeokoka na bado unatenda dhambi? Haitakiwi uwe na doa lolote huu ndio ukweli na usidanganyike ukifa utaombewa ndio uende mbinguni, wakati wako ndio huu wewe uliye hai na MUNGU huwasikiliza walio hai sababu yeye ni MUNGU aliye hai, na kama ni MUNGU aliye hai basi yeye siyo MUNGU wa wafu. Msitende dhambi, jitengeni na tabia za dunia hii. Akaniambia yeye alikufa msalabani na aliubeba msalaba ili wewe usibebeshwe tena msalaba! Watu wote msibebe msalaba maana YESU alishabeba, unapobeba unakuwa unampinga yeye neno lake. Hata mashingoni msivae wala kutembeza katika eneo lolote MSALABA SIYO YESU. Mnatakiwa mumuinue YESU na jina lake na ukuu wake peke yake, ila watu wanainua misalaba kitu ambacho ndicho kilicho muulia YESU; huko ni kumuinua shetani na hata kaburi lake haupaswi kuliinua maana kaburi lake alilozikiwa siyo MUNGU, wala msalaba siyo MUNGU.
Hapa ndipo shetani alipo wateke wanadamu fahamu zao wakajiona wapo salama katika nuru, kumbe wapo katika giza la shetani. Ibada za misalaba, kubeba misalaba shingoni na kuibusu huu ni upofu ulioletwa na shetani ili watu wasiliinue jina la YESU na badala yake fahamu zao na akili zao zikatekwa katika vifaa vilivyomuulia YESU na kuzikwa! Kama ni mwanadamu mwenye akili timamu hata ukifikiria utajiona unakosa kubwa la kumkufuru ROHO MTAKATIFU. Kwanza imeandikwa msiabudu chochote wala kuisujudia kilichotengenezwa na mwanadamu pia hata alivyoviumba MUNGU, ikiwemo nyota, mwezi na vinginevyo. Tazama sasa utaona ulivyotekwa na shetani, ondokeni huko mkatengwe na uovu maana mahali penye sheria hizo ni mahali pa muovu shetani au mpinga kristo.
Anarudi YESU, tazama hata kipindi cha kina Nuhu alitumwa na akayasema tubuni, acheni uovu, wakamcheka wakamtukana na kumuona amechanganyikiwa, nawaeleza tena hivi ndivyo itakavyo kuwa katika KIAMA nawasihi OKOKENI moto ni mkubwa wa jehanamu aliotengenezewa shetani na wale watakaofuata matendo ya shetani (dhambi). Ukibatizwa ubatizo tofauti na aliobatizwa YESU ujue unayo dhambi, usipookoka ujue unayo dhambi tayari maana ameagiza watu wote waokoke na kumpokea yeye. Usipoishi maisha matakatifu ujue ni dhambi. Mimi Hebron mwanzoni sikuyaelewa haya ila aliendelea kunifundisha na mimi nawaeleza ili mpone maana hakuna mwalimu zaidi ya YESU WA NAZARETI na pia uelewe pia ukiona mafundisho tofauti na neno la MUNGU aliye hai uelewe pia mafundisho hayo yanatokea kwa yesu wa kuzimu ambaye ndiye yesu wa uongo hivyo anaingia ndani ya watumishi akawapatia elimu yake ya uongo na wakaisambaza katika makanisa mengi katika ulimwengu huu na watu wakaipokea ile elimu ya uongo. Mfano rahisi elimu ya ubatizo wa maji ya kikombe, tafuta katika biblia yote haupo na kama haupo sasa unatoka wapi? Jibu, unatoka katika kitabu cha yesu wa uongo na watu wote waliobatizwa ubatizo wa kikombe hataenda hata mmoja, sawa sawa na alivyonieleza YESU peke yake, na wewe uwaeleze watu hata uwaforwadie watu ili wapone roho zao na zaidi usome katika kitabu cha UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE, nilichokiandika mimi Nabii Hebron, ingia katika blog na website www.prophethebron.orgutalisoma na pia vipo katika kanisa langu.
Haya ndiye maneno ya MUNGU aliye hai na yapo kwa ajili ya wanadamu wote ila shetani amewavuna mamilioni na kuwajazia elimu ya uongo. Yeye ndiye njia ya ukweli na uzima sasa ndio ukweli wa YESU wa ubatizo unaoufuata au unaompinga na kufuata ubatizo wa uongo? Fuata aliyoagiza peke yake tena lisibadilishwe (Ufunuo 22: 18-19) onyo atakayeongeza au kupunguza atahukumiwa na wote wanaoshiriki maneno ya uongo nao njia ni moja, na hao wote wanaobatiza ubatizo tofauti na alioagiza YESU hao wanaongozwa na mpinga kristo na mwalimu wao ni yesu wa uongo, wala YESU WA NAZARETI hawatambui wala kuwajua. Nawaeleza muelewe hata ukibatizwa katika kisima au ukabatizwa kwa jina la mchungaji ujijue umetekwa na shetani na pia huyo mchungaji amekuteka wewe na wewe ni mtumwa wake milele na hautamuona YESU milele bali utamuona yesu wa uongo maana umekubali maneno yake ya uongo yakakaa ndani yako hivyo anaouhalali wa kukutawala sababu ndani yako umewekewa na wengi hawajui ukweli huu, nawasihii tubuni leo hii.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU MIMI NINA DHAMBI NAOMBA UNISAMEHE UNIANDIKE KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WEWE YESU WA NAZARETI UWE BABA YANGU MILELE. NIPONYE, NIONGOZE WEWE PEKE YAKO KWANZIA SASA, NIFUNGUE FAHAMU ZANGU NIKUJUE WEWE. AMEN.
NOTE:
Soma makala na vitabu katika blog yangu hakika utakua kiroho, na kama hakuna kanisa la kweli mahali ulipo wewe uwe unasoma vitabu nilivyoviandika, na pia uwe unasikiliza mahubiri kwa njia ya YouTube ambayo nimeyahubiri mimi, na usome katika home page ya website uangalie vipindi vya television na redio ujue muda wake uwe unasikiliza na mimi naendelea kuwaombea. Na wote mliopo nchi za nje nawakaribisha kanisani kwangu uje uponywe na ukutane na YESU, zaidi upige simu utaelekezwa jinsi ya kufika au utume email utajibiwa.
Nawatakia wokovu ndani yenu.
NABII HEBRON.
[ad_2]